-->

Mpango wa mafunzo ya TEHAMA

18 Julai 2016

Mpango wa mafunzo ya ICT kwa Walimu wa Sayansi na Hisabati Shule za Sekondari ulianzishwa ili kuwapanulia Walimu wigo wa kujifunza na kufundisha, kutoa wepesi kwa Mwalimu kufanya maandalio ya somo pamoja na kutafuta rejea,

japokuwa imesababisha kuweza kufundisha bila ya kufanya majaribio,hata hivyo imerahisisha kwa sababu mara nyingine mwalimu hukosa vifaa vya kufundishia kwa wakati, ufundishaji kwa ICT umebainisha uwezo wa kutumia muda mfupi kuhifadhi maudhui (Teaching notes) kumwezesha msomaji (mfundishaji kufanya maandalizi au kujisomea bila utegemezi, nia na madhumuni ni kumwezesha mwalimu kufundisha kwa umakini na kumaliza muhtasari wa masomo ipasavyo.

Matumizi ya ICT hutekeleza mpango wa Elimu kwa usawa kwa wote, na kufanya mwanafunzi aweze kuleta/kufikisha maendeleo kwa jamii, na kuweza kuwasiliana.WESTU imetengeneza Sera ya maelekezo kwa matumizi ya ICT katika Elimumsingi, ikifuata yaliyo kwenye Sera,maendeleo ya Sera kwenye mambo yanayohusu maendeleo ya Elimu ikilinganisha Sera ya Taifa ya ICT ya 2003, kwa vile ICT ni elimu mtambuka, Sera imezingatia shughuli za ICT katika Nyanja zote za Elimu ilijumuishwa Elimu ya ufundi, Elimu ya juu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Ili Sera itekelezeke Kitengo cha Elimu ya Sekondari WESTU kimeandaa moduli za kufundishia masomo ya ICT katika kujifunza na kufundishia.

Utafiti ulifanyika ili kubaini uhitaji wa matumizi ya ICT, andiko liliandikwa kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo:

 1. Kukosa uelewano juu ya umuhimu wa matumizi ya ICT katika ufundishaji na ujifunzaji,
 2. Kukosekana kwa misingi Elimu ya matumizi ya ICT,
 3. Kukosekana Elimu juu ya utunzaji wa vifaa vya ICT,
 4. Kukosa Elimu ya msingi kwa matengenezo/marekebisho ya vifaa vya ICT,
 5. Kukosa mbinu za kutumia ili kuoanisha ICT kwenye ujifunzaji na ufundishaji.

Hivyo basi, mada za kufundisha ICT ziliandaliwa kwa kufuata uhitaji.

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…