-->

Mpango wa Maendeleo ya Elimu Sekondari (MMES)

20 Juni 2016

Katika Maendeleo ya Mpango wa Elimu (SEDP) ni mpango mpana wa Elimu unaondeshwa chini ya mwavuli wa ESDP (Education Sector Development Programme), umeendeshwa kwa awamu ya miaka mitano kwa kila awamu.

 Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari AWAMU I (MMES I)

SEDP inatekelezwa na Wadau wa Elimu mbalimbali, kujumuisha Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi (WESTU), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PO-RALG), Halmashauri za Mitaa, Kata, Bodi za Shule Wadau wa Maendeleo ya Elimu pamoja na Benki ya Dunia (W.B).

 SEDP I ilitekelezwa kati ya mwaka 2004 na mwaka 2009 ikiwa na misingi ya kitaifa ya kutoa Elimu ikizingatia mikakati ya Elimu kama vile Mkukuta, ambao ulitekeleza Sera ya Mafunzo ya mwaka 1995 katika Mipango ya Milenia ya Maendeleo ya Malengo ya Elimu ya mwaka 2001 (ESDP, 2001).

Lengo la ujumla la SEDP I ilikuwa kuinua/kuendeleza elimu yenye viwango kwa wote, mapitio (Review) ya utekelezaji wa SEDP I yamefanikisha upatikanaji wa Elimu sawa kwa wote, idadi ya shule za sekondari imeongezeka mara tatu kati ya mwaka 2004 na 2009, na namba ya uandikishaji watoto imepata shuleni kasoro mbalimbali zimerekebishwa japo kuwa kumekuwepo na changamoto za utendaji, idadi ya waalimu imeongezeka, mazingira ya shule na miundombinu imeboreshwa, mbinu za ufundishaji, na uongozaji shule umeboreshwa.

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari  AWAMU II (MMES II)

Maelezo ya Jumla ya Mradi

MMES II ni mradi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia tangu mwaka 2010 . Kwa mujibu wa makubaliano kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lengo kuu la MMES II ni kuinua kiwango cha ubora wa Elimu ya Sekondari kwa kutoa kipaumbele kwenye maeneo yaliyo na mazingira magumu katika utoaji wa elimu. Ili kufikia lengo hilo msisitizo katika utekelezaji umewekwa katika maeneo manne yafuatayo:-

 1. Kuboresha miundombinu ya shule za sekondari 1,200 zilizopo;

Lengo la sehemu hii ni kuongeza idadi ya shule za sekondari zinazokodhi mahitaji ya kimsingi ya miundombinu.

Ili kufikia lengo, mradi hukarabati na kukamilisha miundombinu ya shule iliyopo, na kujenga miundombinu mipya. Kutokana na rasilimali finyu zilizopo, mradi kwa kuzingatia tathmini ya mahitaji, unagharamia ujenzi na usimamizi wa ujenzi wa (i) madarasa, (ii) maabara za sayansi, (iii) nyumba za waalimu, (iv) vyoo, (v) mifumo ya maji, na (vi) umeme (kwa njia ya gridi ya taifa au nishati ya jua). Malengo haya yalitokana na mashauriano ya kina na wadau mbalimbali, ambayo yaliamua kuwa hii ndiyo miundombinu muhimu kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji  na na ujifunzaji katika shule.

 1. Kuhakikisha kuwepo kwa walimu wa kutosha na ubora wa ufundishaji na ujifunzaji hususani katika masomo ya Hisabati, Sayansi na Lugha;

Malengo ya sehemu hii ni uboreshaji wa upelekaji wa walimu katika shule zilizoko maeneo ya vijijini; kuboreshwa kwa ufundishaji na ujifunzaji katika masomo ya Hisabati, Sayansi, na Lugha; na kuboresha mbinu za kufundishia na kujifunzia. Mafanikio ya malengo hapo juu yana vihashiria vifuatavyo: (i) upatikanaji wa walimu unaopimwa kwa idadi ya walimu wenye sifa katika shule zilizoko katika mazingira magumu ya utoaji wa elimu na (ii) ongezeko la usambazaji wa walimu wa Hisabati na Sayansi linalopimwa na uandikishaji wa wanafunzi-walimu wa kozi za kufundisha Hisabati na Sayansi katika vyuo vya ualimu TTCs).

 1. Kuhakikisha upatikanaji na matumizi sahihi ya rasilimali fedha kwenye shule kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia;

Lengo ni kuhakikisha kuwa fedha za kutosha zinatolewa kwa shule za sekondari (kwa sasa ni Tsh. 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka) na zinatolewa kwa wakati, na kufuatiliwa kwa ufanisi. Malengo haya yamekuwa yakifikiwa kwa njia ya kuboresha utoaji vitabu vya kiada na kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi (kwa mfano, vifaa vya mwalimu, miongozo ya waalimu; vifaa vya maabara, vifaa na kemikali).

 1. Kujenga uwezo wa Wakala na Taasisi za Elimu ili kutekeleza mageuzi ya kielimu yaliyopo na yale yajayo

Lengo ni kuimarisha uwezo wa wakala na taasisi kwa ajili ya usimamizi wa elimu; taasisi hizi ni ADEM, TIE na NECTA. Rasilimali endelevu kuimarisha uwezo wa mipango, uongozi, utoaji, ufuatiliaji na usimamizi wa elimu ni muhimu kwa kuboresha ubora na ufanisi wa utoaji huduma za elimu. Pia sehemu hii imehusika na upanuzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Elimu ambao unawezesha upatikanaji wa takwimu muhimu za elimu kwa urahisi na ambazo ni sahihi na rahisi kuchakata; kupatikana takwimu kwa urahisi na kwa wote ni muhimu kwa kufanya maamuzi na kukuza uwazi na ufanisi.

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…