Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akipata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa utafiti kwenye chumba maalumu cha maabara ya mazao kama vile mbegu ya viazi vitamu, mbegu mpunga na muhogo visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Naibu waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia mhandisi Stella Manyanya akikagua moja ya miradi ya ufugaji wa kasa  inayotekelezwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia, COSTECH kisiwani Unguja ambapo naibu waziri amewaka watafiti kufanya tafiti ambazo zitaleta matokeo katika jamii na siyo tafiti kuishia kwenye vitabu. Pia Naibu waziri amesisitiza kuwepo kwa wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na  na kuongeza fedha kwa ajili ya taifiti hizo.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akifanya mazungumzo na Waziri wa Elimu na Amali wa Zanzibar Riziki Pembe Juma hivi karibuni mjini Unguja ambapo wote kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya Elimu.

Waziri  Wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia maelezo yanayotolewa na wabunifu mbalimbali waliopo katika atamizi wakati alipotembelea Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Waziri aliitembelea Taasisi hiyo ili kuona jinsi inavyofanya kazi zake

Waziri  WaElimu, Sayansi na Teknlojia Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia maelezo yanayotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Dkt. Hassani Mashinda. Waziri aliitembelea Taasisi hiyo ili kuona jinsi inavyofanya kazi zake

Kurasa 2 ya 24

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…