Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti mmoja wa vijana wazalendo waliojitolea kwa ajili ya kufyatua tofari 45,000 katika kipindi cha mwezi mmoja ili kujenga nyumba za walimu, vyumba vya madarasa na mbweni katika shule ya Sekondari ya Nasibugani iliyopo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na washiriki wa tamasha la uzinduzi wa kitabu cha ufugaji na mabadiliko ya Tabia Nchi katika nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja, walioketi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish (Kushoto) mara baada ya kuzindua kitabu kinachoonyesha ufugaji na mabadiliko ya Tabia Nchi katika nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua kitabu kinachoonyesha ufugaji na mabadiliko ya Tabia Nchi katika nchi za Afrika Mashariki ambapo amesema mabadiliko hayo si hadithi na kwamba jitihada zinahitajika katika kutunza mazingira. Aliyepo upande wa kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Rwekaza Mkandara na upande wa kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya, uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya leo amezindua programu mpya inayojulika kama jiandalia ajira, (via) katika ukumbi wa Jullius Nyerere uliopo jijini Dar es salaam.