Katibu Mkuu Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akizungumza na watendaji wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara.
Makatibu Wakuu wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hizo mara baada ya makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Majengo Tanzania Elius Mwakibinga akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera, huku Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani akishuhudia. Shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akiwa ameshika ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Bukoba Vijijini Mwantumu Dau na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani ambaye yeye pamoja na wadau wengine wamejitolea kusaidia kukarabati baadhi ya miundombinu ya shule hiyo. Shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila kwa pamoja wakiwa wamebeba tofari walilotengeneza wenyewe ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kuunga mkono juhudi za vijana wazalendo waliojitolea kwa ajili ya kufyatua tofari 45,000 katika kipindi cha mwezi mmoja ili kujenga nyumba za walimu, vyumba vya madarasa na mabweni katika shule ya Sekondari ya Nasibugani iliyopo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.