Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na Mwakilishi mkazi wa benki ya Dunia Bella Bird kuhusu mchango wa benki ya Dunia katika Maendeleo ya Sekta ya Elimu hapa nchini. Bella Bird anawakilisha nchi za Tanzania,Burundi, Malawi na Somalia.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti mmoja wa walimu aliyehitimu mafunzo ya Astashahada ya uongozi na usimamizi wa Elimu kwa njia ya masafa[CELMA-ODL], hivi karibuni mkoani MBEYA.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na walimu waliohitimu mafunzo ya Astashahada ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa[CELMA-ODL]]Kwa walimu wakuu Zaidi ya 800 kutoka shule za msingi katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, na Songwe. [walimu hawapo pichani].
waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi ya BUSOHKELO wakiwa katika darasa linaloongea. Kwa mujibu wa walimu wanaofundisha darasa la kwanza na la pili wameeleza kuwa darasa linaloongea limewsaidia wanafunzi kusoma, kuandika na kuhesabu kwa urahisi Zaidi [KKK] shule ya msingi ipo Wilayani RUNGWE mkoani MBEYA.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na mkandarasi anaesimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya chuo cha Ualimu cha MPUGUSO, kilichopo wilayani Rungwe mkoani MBEYA ambapo waziri Ndalichako amemtaka mkandarasi kuzingatia viwango vya ujenzi ili majengo yadumu kwa muda mrefu.