Jumatatu, 02 Oktoba 2017 07:58

SERIKALI YA TANZANIA NA HUNGARY ZATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO SEKTA YA ELIMU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce  Ndalichako amesaini  mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano  katika Sekta ya Elimu Kati ya Tanzania na Hungary, mjini Budapest nchini Hungary.
Mkataba huo utaanza kutekelezwa Januari 1 mwakani ambapo Tanzania itapata uhisani wa nafasi 30  kila mwaka kwa mwaka 2018, 2019 na 2020. 
 
Ufadhili huo utahusu  shahada ya kwanza nafasi 10 katika fani za Kilimo, Uhandisi, Sayansi Asili na ya Uchumi, katika ngazi ya Shahada ya Uzamili nafasi 15 fani za Kilimo, Uhandisi, Sayansi Asili na ya Uchumi; na
nafasi 5 katika ngazi ya Uzamivu katika eneo ambalo Tanzania itahitaji.
 
Kwa upande wake, Tanzania itaangalia uwezekano wa kupokea wanafunzi katika ngazi ya shahada ya pili na uzamivu kutoka Hungary kwa uhisani usiozidi mwezi mmoja, kwa ajili mafunzo ya muda mfupi kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kitaalam na utafiti.
 
Kabla ya utiaji saini kwa mkataba huu, Waziri Ndalichako  aliishukuru Serikali ya Hungary kwa uhisani wa nafasi hizo za masomo kwa ajili ya watanzania pia  alifikisha salamu na shukrani za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli kwa Serikali ya Hungary, kutokana na uhisani wa nafasi hizo 30, ambapo awali, Hungary walikuwa wametoa nafasi 10 kwa mwaka.
 
Utiaji saini Makubaliano hayo pia ulihudhuriwa na Dkt. Laszolo Palskovics, Waziri wa Uwezeshaji Rasilimaliwatu wa nchini Hungary.
 
 
Katika ziara hiyo ya siku mbili nchini humo Waziri Ndalichako alitembelea Vyuo Vikuu vitatu na chuo kimoja cha ufundi kwa lengo la kujionea na kupata uzoefu, pamoja na   kubadilishana uzoefu hasa ukizingatia kuwa Tanzania ipo katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda.
 
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano, Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

 

Read 51671 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…