Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

 • Lengo

  Kuhakikisha kunawepo  na sera zilizo bora na madhubuti za kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji ili kuimarisha usawa wa kujiunga, ubora na kuongeza fursa sawa  za mafunzo na stadi zitolewazo.

  MAJUKUMU  

  • Kufuatilia mara kwa mara mwenendo wa hali ya ujuzi katika soko la ajira na kupata taarifa ili kubainisha maeneo ambayo yatahitaji kutolewa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
  • Kuendeleza ufundishaji na ujifunzaji, utafiti na ubunifu ulio ubora, wa hali ya juu na wa ushindani kwa kiwango cha kimataifa.
  • Kutoa taarifa kwa ajili ya kuandaa, kufuatilia, kutathmini mipango na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango na miradi ya wizara kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuwasiliana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Baraza  la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Bodi nyingine za Kitaalamu kwa lengo la kuwezesha kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yaliyo bora.
  • Kuendeleza na kujenga ushirikiano endelevu wa kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuimarisha mahusiano ya karibu ya utendaji kazi na Wizara inayoshughulikia masuala ya vyuo vya maendeleo ya wananchi pamoja na maendeleo ya jamii kuhusu mafunzo ya ufundi stadi katika  ngazi ya jamii;
  • Kuhamasisha umma juu ya majukumu na kazi za sekta ndogo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia utekelezaji wa shughuli za taasisi/vyuo vinavyowajibika kwa Idara.

   Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa Seksheni mbili zifuatazo:

  • Elimu ya Ufundi na Mafunzo; na
  • Mafunzo ya Ufundi Stadi. 

   

 • Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo

   

  Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

  • Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo, kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ilikutoa kwa ufanisi wa elimu ya ufundi mafunzo.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
  • Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu elimu ya ufundi na mafunzo ikiwemo ugharamiaji.
  • Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ambapo Tanzania ni mwanachama.
  • Kuandaa kila mwaka Fora ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa kushirikiana na wadau.
  • Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa elimu ya ufundi na mafunzo, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
  • Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo nchini.
  • Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo, viwanda na biashara.
  • Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo vilivyo chini ya Wizara.
  • Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya elimu ya ufundi na mafunzo kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa elimu ya ufundi na mafunzo kwa nchi za nje na kikanda.
  • Kutafuta taarifa za wahitimu wa elimu ya ufundi na mafunzo, kuandaa na kuziboresha kuhusu ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
  • Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kadri zinavyohitajika.

  Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

 • Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi

   

  Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

  • Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi,kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ili kutoa kwa ufanisi mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi  kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
  • Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji.
  • Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu mafunzo ya ufundi stadi ambapo Tanzania ni mwanachama.
  • Kuandaa kila mwaka Fora ya Wadau wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kushirikiana na wadau.
  • Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa mafunzo ya ufundi stadi, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
  • Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi nchini.
  • Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi, viwanda na biashara.
  • Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi vilivyo chini ya Wizara.
  • Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya mafunzo ya ufundi stadi kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa nchi za nje na kikanda.
  • Kutafuta taarifa za wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi, kuandaa na  kuziboresha kuhusu  ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
  • Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi kadri zinavyohitajika.

   Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

   

Read 23917 times

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…