Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo wanafunzi wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la  Elimu la Mafunzo ya Ufundi

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mtakumbuka tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa sayansi walitakiwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia NACTE, lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa vijana hao wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, Wizara imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali” Alifafanua Dkt. Akwilapo Naibu Katibu Mkuu Elimu.

Aliendelea kusema kuwa wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa wakisomea stashahada ya ualimu wa Msingi.

Dkt. Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi hao wamepangiwa vyuo vya ulaimu vya Marangu na Tabora.

Aidha, Dr Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na serikali. Pia amewataka kutembelea Tovuti ya Wizara ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona  vyuo walivyopangiwa.

Mnamo tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma.  Katika mchujo wa awamu ya Kwanza wanafunzi 382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo katika  Chuo Kikuu cha Dodoma na wengine 4586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya serikali. 

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na Wawakilishi kutoka kamati ya Global Partnership for Education  wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara 

Majina ya wanachuo waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma waliopangiwa kurudi kwenye chuo hicho, wanaokwenda kwenye vyuo vya ualimu na ambao hawana vigezo vya kujiunga na vyuo hivyo.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia hivi karibuni ilitoa uamuzi kuhusu wanachuo 7,805 waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

The Government of the United Republic of Tanzania has received fully funded scholarships from the Republic of Tunisia, and is hereby requesting qualified Tanzanians to apply for ‘’Fundamental Degree in Computer Science’’

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…