Katika Maendeleo ya Mpango wa Elimu (SEDP) ni mpango mpana wa Elimu unaondeshwa chini ya mwavuli wa ESDP (Education Sector Development Programme), umeendeshwa kwa awamu ya miaka mitano kwa kila awamu.

 • Lengo

  Kuhakikisha kunawepo  na sera zilizo bora na madhubuti za kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji ili kuimarisha usawa wa kujiunga, ubora na kuongeza fursa sawa  za mafunzo na stadi zitolewazo.

  MAJUKUMU  

  • Kufuatilia mara kwa mara mwenendo wa hali ya ujuzi katika soko la ajira na kupata taarifa ili kubainisha maeneo ambayo yatahitaji kutolewa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
  • Kuendeleza ufundishaji na ujifunzaji, utafiti na ubunifu ulio ubora, wa hali ya juu na wa ushindani kwa kiwango cha kimataifa.
  • Kutoa taarifa kwa ajili ya kuandaa, kufuatilia, kutathmini mipango na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango na miradi ya wizara kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuwasiliana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Baraza  la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Bodi nyingine za Kitaalamu kwa lengo la kuwezesha kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yaliyo bora.
  • Kuendeleza na kujenga ushirikiano endelevu wa kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuimarisha mahusiano ya karibu ya utendaji kazi na Wizara inayoshughulikia masuala ya vyuo vya maendeleo ya wananchi pamoja na maendeleo ya jamii kuhusu mafunzo ya ufundi stadi katika  ngazi ya jamii;
  • Kuhamasisha umma juu ya majukumu na kazi za sekta ndogo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia utekelezaji wa shughuli za taasisi/vyuo vinavyowajibika kwa Idara.

   Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa Seksheni mbili zifuatazo:

  • Elimu ya Ufundi na Mafunzo; na
  • Mafunzo ya Ufundi Stadi. 

   

 • Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo

   

  Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

  • Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo, kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ilikutoa kwa ufanisi wa elimu ya ufundi mafunzo.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
  • Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu elimu ya ufundi na mafunzo ikiwemo ugharamiaji.
  • Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ambapo Tanzania ni mwanachama.
  • Kuandaa kila mwaka Fora ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa kushirikiana na wadau.
  • Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa elimu ya ufundi na mafunzo, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
  • Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo nchini.
  • Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo, viwanda na biashara.
  • Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo vilivyo chini ya Wizara.
  • Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya elimu ya ufundi na mafunzo kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa elimu ya ufundi na mafunzo kwa nchi za nje na kikanda.
  • Kutafuta taarifa za wahitimu wa elimu ya ufundi na mafunzo, kuandaa na kuziboresha kuhusu ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
  • Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika elimu ya ufundi na mafunzo.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kadri zinavyohitajika.

  Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

 • Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi

   

  Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

  • Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi,kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ili kutoa kwa ufanisi mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi  kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
  • Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji.
  • Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu mafunzo ya ufundi stadi ambapo Tanzania ni mwanachama.
  • Kuandaa kila mwaka Fora ya Wadau wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kushirikiana na wadau.
  • Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa mafunzo ya ufundi stadi, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
  • Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi nchini.
  • Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi, viwanda na biashara.
  • Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi vilivyo chini ya Wizara.
  • Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya mafunzo ya ufundi stadi kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
  • Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa nchi za nje na kikanda.
  • Kutafuta taarifa za wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi, kuandaa na  kuziboresha kuhusu  ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
  • Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika mafunzo ya ufundi stadi.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi kadri zinavyohitajika.

   Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

   

LENGO

Kuhakikisha kunawepo  na sera zilizo bora na madhubuti za kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji ili kuimarisha usawa wa kujiunga, ubora na kuongeza fursa sawa  za mafunzo na stadi zitolewazo.

MAJUKUMU  

 1. Kufuatilia mara kwa mara mwenendo wa hali ya ujuzi katika soko la ajira na kupata taarifa ili kubainisha maeneo ambayo yatahitaji kutolewa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
 2. Kuendeleza ufundishaji na ujifunzaji, utafiti na ubunifu ulio ubora, wa hali ya juu na wa ushindani kwa kiwango cha kimataifa.
 3. Kutoa taarifa kwa ajili ya kuandaa, kufuatilia, kutathmini mipango na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
 4. Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango na miradi ya wizara kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
 5.  Kuwasiliana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Baraza  la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadina Bodi nyingine za Kitaalamu kwa lengo la kuwezesha kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yaliyo bora.
 6. Kuendeleza na kujenga ushirikiano endelevu wa kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
 7. Kuimarisha mahusiano ya karibu ya utendaji kazi na Wizara inayoshughulikia masuala ya vyuo vya maendeleo ya wananchi pamoja na maendeleo ya jamii kuhusu mafunzo ya ufundi stadi katika  ngazi ya jamii;
 8. Kuhamasisha umma juu ya majukumu na kazi za sekta ndogo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
 9. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za taasisi/vyuo vinavyowajibika kwa Idara.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa Seksheni mbili zifuatazo:

 1. Elimu ya Ufundi na Mafunzo; na
 2. Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo

Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

 1. Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo, kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ilikutoa kwa ufanisi wa elimu ya ufundi mafunzo.
 2. Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
 3. Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu elimu ya ufundi na mafunzo ikiwemo ugharamiaji.
 4. Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo ambapo Tanzania ni mwanachama.
 5. Kuandaa kila mwaka Fora ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa kushirikiana na wadau.
 6. Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa elimu ya ufundi na mafunzo, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
 7. Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
 8. Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo.
 9. Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza elimu ya ufundi na mafunzo nchini.
 10. Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo, viwanda na biashara.
 11. Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo vilivyo chini ya Wizara.
 12. Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya elimu ya ufundi na mafunzo kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
 13. Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
 14. Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu elimu ya ufundi na mafunzo.
 15. Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa elimu ya ufundi na mafunzo.
 16. Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo.
 17. Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa elimu ya ufundi na mafunzo kwa nchi za nje na kikanda.
 18. Kutafuta taarifa za wahitimu wa elimu ya ufundi na mafunzo, kuandaa na kuziboresha kuhusu ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
 19. Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya elimu ya ufundi na mafunzo.
 20. Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika elimu ya ufundi na mafunzo.
 21. Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kadri zinavyohitajika.

Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi

Seksheni hii itafanya shughuli zifuatazo:

 1. Kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi,kufuatilia, kutathmini na kushauri juu ya utekelezaji kwa kutegemea taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo na za wataalamu pamoja na taasisi/ vyuo vinavyotoa mafunzo ili kutoa kwa ufanisi mafunzo ya ufundi stadi.
 2. Kuandaa, kuchambua na kuwezesha kupatikana kwa taarifa zinazohusu Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi  kulingana na mtiririko wa kazi na itifaki husika  kwa  ajili ya Mfumo wa Kutunza Taarifa za Masuala ya Sekta ya Elimu na Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi.
 3. Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya uchambuzi na kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kuhuisha utekelezaji wa sera mbalimbali za elimu zinazohusu mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo ugharamiaji.
 4. Kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na viambata vyake pamoja na masuala ya mahusiano ya kikanda na kimataifa kuhusu mafunzo ya ufundi stadi ambapo Tanzania ni mwanachama.
 5. Kuandaa kila mwaka Fora ya Wadau wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kushirikiana na wadau.
 6. Kuhamasisha umma juu ya fursa zilizopo kwa mafunzo ya ufundi stadi, uchangiaji gharama za uendeshaji mafunzo, urejeshwaji mikopo, sera za ugharamiaji na uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.
 7. Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya utekelezaji kuhusu mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya matumzi katika michakato ya maendeleo ya sera.
 8. Kubuni, kuandaa na kuimarisha mahusiano na mikataba ya kiutamaduni na kimaendeleo kuhusu mafunzo ya ufundi stadi.
 9. Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi nchini.
 10. Kubuni, kuandaa na kuanzisha au kuendeleza programu kwa ajili ya ushirikiano endelevu kati ya taasisi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi, viwanda na biashara.
 11. Kusimamia na kuendeleza maendeleo ya taasisi/vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi vilivyo chini ya Wizara.
 12. Kubuni na kusanifu uanzishwaji wa taasisi/vyuo vipya vya mafunzo ya ufundi stadi kulingana na mahitaji ya ujuzi ya kitaifa.
 13. Kubuni, kuandaa na kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na kitaalamu kwa watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
 14. Kuendeleza na kuhamasisha usawa, ubora na fursa sawa katika kutoa kwa gharama nafuu mafunzo ya ufundi stadi.
 15. Kushawishi, kuendeleza, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa mara kwa mara wa skolashipu, mikopo, na misaada ya hali na mali kwa wanafunzi na watumishi wa mafunzo ya ufundi stadi.
 16. Kusimamia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na watumishi katika taasisi/vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi.
 17. Kutunza na kuboresha daftari za skolashipu na ugharamiaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa nchi za nje na kikanda.
 18. Kutafuta taarifa za wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi, kuandaa na  kuziboresha kuhusu  ya hali ya ajira zao ikiwemo ujuzi unahohitajika katika soko kwa ajili kushauri taasisi za kusimamia ubora wa mafunzo,   za ubora wa wahitimu na pia viwanda na biashara.
 19. Kushauri juu ya vigezo, kanuni na taratibu za skolashipu, misaada na mikopo ya mafunzo ya ufundi stadi.
 20. Kuwezesha upatikanaji wa vibali vya kuishi nchini kwa walimu/wakufunzi na wanafunzi wa kigeni na watumishi wa kujitolea kutoka nje ya nchi katika mafunzo ya ufundi stadi.
 21. Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Idara kulingana na miongozo ya kazi na itifaki ya Seksheni ya Mafunzo ya Ufundi Stadi kadri zinavyohitajika.

Seksheni  hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

 • Dira

  Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuwezakuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa."

   

 • Dhima

  "Kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu."

TARATIBU ZA KUANZISHA NA KUSAJILI SHULE

Ili kuanzisha na kusajili Shule yenye ubora unaostahili wadau hawana budi kufuata hatua mbalimbali kama zilivyoainishwa kwa kina katika “Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982”.  Kwa kifupi hatua hizo ni kama.

 • Hatua ya kwanza:  Kibali cha  Kujenga Shule

  Mwenye nia na uwezo wa kuanzisha Shule atume maombi ya kutaka kujenga shule kwa maandishi kwa Afisa Elimu

  Kiongozi.  Maombi haya yapitishwe kwa Afisa Elimu  wa Wilaya Shule itakapojengwa na Afisa Elimu  Mkoa yakiwa na viambatisho vifuatavyo: 

  • Rejea mwongozo wa andiko la mradi la Wizara, Bank Statement yenye zaidi y ash. Milioni 62,000,000/=  Nakala ya hati/offer/uthibitisho wa kumiliki ardhi iliyotolewa kwa matumizi ya shule inayotambu8lika kisheria na serikali kuu ya mtaa au kijiji ( eneo lisipungue ekari 71/2  kijijini na 31/2 mjini) Michoro ya majengo ya shule inayoonyesha vipimo kwa kuzingatia viwango vya Wizara na Elimu ya mafunzo ya ufundi, Ramani ya shule inayoonyesha mpangilio wa majengo na viwanja vya michezo, Cheti cha usajili wa kampuni, shirika , umoja , NGO iwapo shule ni ya jumuia na katiba yake au mkataba wa maridhiano. Endapo mdau anataka ikutumia jina la Mtakatifu ( Saint ) awasilishe kibali toka kwa askofu wa dini inayotambulika kinachoidhinisha matumizi ya jina hilo.
  • Kamishina wa Elimu akiridhika na maombi hayo atatoa kibali cha kujenga Shule kimaandishi, ndipo ujenzi utaanza.

 • Hatua ya pili: Kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na Meneja wa Shule

  Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na inahusisha yafuatayo:

  • Mwombaji ajaze fomu Na. RS. 6 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na RS. 7 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Meneja wa Shule.  Hatua hii itafanywa baada ya mwombaji kuwa amekamilisha ujenzi wa majengo yote  muhimu kwa asilimia 75% Majengo hayo ni vyumba vya madarasa, Jengo la utawala/Ofisi za walimu, Maktaba, vyoo vya wasichana, wavulana na wafanyakazi bwalo/ukumbi,  maabara. Majengo hayo lazima yawe yamekaguliwa na mamlaka za Wilaya, ambazo ni ; Mhandisi wa Majengo , Afisa Afya na Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Wilaya na kwamba fomu hizo ziwe zimepitishwa na  Afisa  Elimu wa Wilaya, Afisa Elimu wa Mkoa na  Katibu Tawala wa Mkoa.
  • Wizara ikiridhika itatoa kibali cha maandishi cha kumthibitisha Mwenye Shule na Meneja wa Shule.

 • Hatua ya Tatu:  Maombi ya Kusajili Shule

  Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na ya pili na inahusisha yafuatayo:

  •  Mwenye Shule hujaza fomu Na. RS 8 ya maombi ya kusajili shule baada ya kuwa amekamilisha mahitaji yote yanayotakiwa kwa Shule ya aina anayoiomba: ambayo ni  Majengo na Samani, Vitabu, Mihutasari ya masomo, Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia na Kuajiri walimu na wafanyakazi wengine wenye sifa na uzoefu.
  • Mwenye Shule ambaye Shule yake imetimiza vigezo vyote na shule kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda hupewa taarifa ya kusajiliwa kwa Shule yake kimaandishi.  Aidha, atapatiwa cheti cha usajili chenye namba ya usajili .

  Usajili wa Shule za Kimataifa

  Wizara husajili shule zenye hadhi ya kimataifa, usajili huo unafanywa na Taasisi za kimataifa zinazosajili Shule za aina hiyo.  Wizara huthibitisha na kutambua shule zinazosajiliwa na taasisi hizo kama za kimataifa.  Taasisi hizo ni “European Council for International Schools” (E.C.I.S) na “Association of International Schools in Africa (AISA).  Taasisi hizo zimeweka vigezo vya

  kusajili Shule za kimataifa.  Shule itapewa usajili pale tu itakapotimiza vigezo vyote vilivyowekwa.

  Hatua za kufuata ili Shule iwe ya Kimataifa

  Mwenye Shule yeyote anayetaka Shule yake iwe na hadhi ya kimataifa anapaswa kufuata hatua zifuatazo:

  • Shule isajiliwe na Wizara kama shule ya kawaida.
  • Mwenye Shule aiombe Wizara kimaandishi kutaka Shule yake iwe ya kimataifa.
  • Endapo Wizara itaridhika na ombi hilo itatoa kibali cha maandishi na Mwenye Shule ataendelea na hatua za kutuma maombi kwenye taasisi zinazosajili shule hizo.
  • Shule itakaposajiliwa kama ya kimataifa, Mwenye Shule aijulishe Wizara kimaandishi na kuambatisha nakala ya usajili huo.

  Usajili wa shule/Taasisi za kidini

  Taasisi za kidini zinazotaka kuanzisha na kuendesha Shule/Taasisi za kidini zinapaswa kufuata hatua zote tatu kama zilivyoelezwa isipokuwa wanapaswa kujaza fomu Na. RS.9 katika hatua ya usajili.

  Tanbihi

  Uvunjaji wa Sheria kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kifungu cha 59.

  Ni nani anayehusika katika mchakato wa usajili wa shule?

  • Katika ngazi ya Wilaya:

  Wakaguzi wa Shule; Maafisa Elimu; Wahandisi wa Majengo na Maafisa Afya wana wajibu mkubwa wa kuthibitisha kuwa maandalizi ya kutosha kuhusu majengo na mazingira ya Shule kiafya yanafaa kwa matumizi ya shule.  Taarifa zinazoandaliwa na watendaji hao husaidia kutoa picha halisi ya matayarisho na kutoa mapendekezo sahihi pale wanapopitisha fomu za maombi ya kumiliki na kuendesha shule.  Maombi haya huisaidia Wizara kupata picha halisi kuhusu matayarisho ya mwombaji na kufanya uamuzi sahihi.

  • Watendaji wa Serikali ya Kijiji/Mtaa na Kata

  Hutoa taarifa mahsusi zinazosaidia kutoa picha ya mahitaji ya Elimu katika eneo lao na kumthibitisha anayetaka kuanzisha Shule kama ndiye mmiliki halali wa eneo la Shule itakapojengwa.

  • Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda

  Hufanya ukaguzi maalumu kwa lengo la kusajili shule na hukamilisha fomu Na RS. 8 kisha kutuma fomu hizo kwa Kamishina wa Elimu pamoja na taarifa ya Ukaguzi wa Shule husika.  Mkaguzi Mkuu wa Shule husimamia na kutathimini utekelezaji wa mitaala pamoja na uendeshaji wa shule kwa ujumla.

  • Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya

  Husimamia masuala yote ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao.  Wanajukumu la kutoa maamuzi juu ya aina ya mipango inayotakiwa kufanywa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za serikali za msingi na za sekondari.  Wanasimamia uhamasishaji wa maendeleo ya sekta ya elimu ya jamii inayowazunguka pia wanapokea na kupendekeza maombi ya kutaka kumiliki, kuendesha na kusajili Shule.

  • Waziri wa Elimu,

  Waziri wa Elimu humthibitisha Mwenye Shule na huidhinisha usajili wa Shule za dini.

 • Usajili wa Walimu

  Usajili wa walimu unafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 sehemu ya VI na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 pamoja na Kanuni ya Elimu ya mwaka 2002.

  Makundi matatu ya walimu yanayoweza kusajiliwa

  • Mwalimu aliyefuzu na kufaulu mitihani kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Mtu asiye na taaluma ya Ualimu atakayeomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.
  • Walimu wasio raia wa Tanzania waliofuzu taaluma ya Ualimu wanaoomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.

  Walimu wenye sifa

  • Mwalimu mwenye sifa husaini mkataba na mwajiri wake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi za Walimu za mwaka 2003
  • Mwalimu huyu husajiliwa kutoka rejesta Na. II kama mwalimu anayesubiri kuthibitishwa.
  • Baada ya kumaliza muda wa kusuburi kuthibitishwa kwa mwaka mmoja,  mwalimu huthibitishwa kwenye rejesta Na. I ya walimu waliothibitishwa kazini.

  Walimu walio na taaluma ya ualimu ambao sio watanzania wanaotaka kufundisha nchini

  • Mwombaji ataomba kupatiwa leseni ya kufundisha kupitia kwa uongozi wa shule anayotaka kufundisha na kuyapitisha maombi hayo kwa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda.  Mwombaji anaambatisha vyeti vya taaluma na umri wake.
  • Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda. hupitia na kutoa mapendekezo ya maombi hayo kwa Kamishina wa Elimu
  • Maombi ya ajira ya Walimu huchambuliwa na kamati maalum ambayo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala kisha humshauri Waziri kupitisha maombi haya.
  • Waziri akiridhika hutoa kibali cha kufundisha nchini.
  • Kamishina wa Elimu  hutoa idhini ya mwombaji kupatiwa leseni.
  • Walimu wenye leseni wanasajiliwa kwenye rejesta Na. III
 • Mwongozo wa Usajili wa Shule 1982

  Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982 unapatikana katika Ofisi za Elimu za Wilaya, Mkoa na Makao Makuu ya Wizara.  Mwongozo huu unatoa tafsiri ya Sheria ya Elimu na Kanuni za Elimu kuhusu usajili wa shule na walimu.

  Mambo muhimu yaliyopo katika mwongozo ni pamoja na fomu za usajili wa shule na walimu.  Aina ya fomu (majina mapya katika mabano) hizo ni:

  • Fomu Na.6 (RS 6) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Mwenye Shule na fomu Na. 7 (RS 7) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Meneja wa Shule.
  • Fomu Na. 8 (RS 8) kuhusu maombi ya usajili wa shule zisizo za Serikali na Fomu Na. 9 (RS 9) kuhusu maombi ya leseni na usajili wa Shule/Taasisi za Dini.
  • Fomu Na. 4 (RT 4) kuhusu maombi ya kutaka kupatiwa leseni za kufundisha.
  • Fomu Na, 3 (RS 3) kuhusu taarifa ya kusajiliwa walimu wenye leseni katika rejesta Na. 3
  • Fomu Na. 1 (RT 1) kuhusu cheti na taarifa ya kusajiliwa walimu ambao wamemaliza muda wa mwaka mmoja na kusubiri kuthibitishwa kazini. 

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…