Jumapili, 12 Januari 2020 23:29

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Januari 11,2020 ameweka jiwe la Msingi katika
*Skuli Mwanakwerekwe
Zanzibar.

Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi imehudhuriwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

Akihutubia wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo Rais John Pombe Magufuli ameipongeza Serikali ya Awamu ya Saba kwa Miaka tisa kwa kuiletea Maendeleo Zanzibar ikiwemo Sekta ya Elimu, huku akiwataka Viongozi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia katika kuongeza ufaulu wa Shule za visiwani katika mitihani ya kitaifa.

Amesema katika kipindi cha miaka tisa idadi ya wanafunzi imeongezeka katika skuli za Maandalizi kutoka 238 mwaka 2010 na kufikia Wanafunzi 382 kwa mwaka 2018 kwa upande wa Sekondari idadi imefikia Wanafunzi 381 kutoka 299 mwaka 2010 na Vyuo Vikuu kutoka 767 mwaka 2010 na kufikia Wanafunzi 3,624 mwaka 2018.

Skuli ya Mwanakwerekwe inajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.628 ambazo ni Mkopo wa Dola milioni 35 ambazo ni zaidi Bilioni 80 kutoka Benki ya Dunia na zimejenga skuli mbalimbali ikiwemo Mwanakwerekwe.

Alhamisi, 19 Desemba 2019 18:11

Serikali imezindua mradi wa ujenzi wa majengo mapya yenye thamani ya Sh. Bilioni 37 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia (World Bank).

Alhamisi, 12 Desemba 2019 16:45

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amewataka Wakuu wa Shule zote za sekondari nchini kuwahimiza wanafunzi wao kushiriki katika mashindano ya uandishi wa insha za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Jumanne, 10 Desemba 2019 16:33

Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema tafiti zinazofanyika nchini zinatakiwa kujibu changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania na Afrika kwa ujumla.

Alhamisi, 28 Novemba 2019 15:39

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezindua chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani Kagera kilichojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 281.

Ujenzi wa Chuo hicho ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kushirikiana na jamii kufikisha Elimu ya Ufundi karibu na Wananchi pamoja na kujenga Vyuo vya VETA katika kila Wilaya nchini ifikapo mwaka 2020, ambapo Wizara imetenga zaidi ya Sh. bilioni 40 katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya VETA katika Wilaya 25 nchini.

Ujenzi wa Chuo cha Ndolage ulianzishwa na Wananchi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Charles Mwijage ambapo wananchi walitoa kiwanja na kuanza ujenzi wa madarasa kwa kutumia michango yao.

Akizungumza katika hafla hiyo Profesa Ndalichako amewataka VETA kuhakikisha wanajenga majengo yote yanayohitajika katika Chuo hicho kwa kutumia mapato ya ndani ya VETA.

"Nimezindua Chuo hiki lakini sijaridhishwa na majengo, ni machache na hayana hadhi kwani Wizara imetoa hela kulingana na mahitaji yenu, inakuwaje bado kuna changamoto za majengo? Natoa miezi sita mkamilishe kwa fedha zenu," alisisitiza Ndalichako.

Alhamisi, 28 Novemba 2019 12:39

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera na kusema kuwa ujenzi wa chuo hicho ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kunakuwa na Vyuo vya ufundi stadi vya Mikoa na Wilaya.

Jumatatu, 25 Novemba 2019 16:57

Serikali ya Tanzania inatekeleza Mradi wa unaolenga kuleta mapinduzi katika Elimu ya Ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Alhamisi, 14 Novemba 2019 14:55

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo imejizatiti na ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba inaondoa fikra potofu kuhusiana na masuala ya kijinsia.

Alhamisi, 14 Novemba 2019 09:40

Serikali kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imetumia kiasi cha shilingi milioni 286.6 kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu katika shule ya msingi Buhangija ya Mkoani Shinyanga.

Jumapili, 10 Novemba 2019 06:53

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako leo Novemba 9, 2019 amefungua majengo ya ofisi mpya za Uthibiti Ubora wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa ofisi hizo Waziri Ndalichako amewataka wathibiti Ubora wa Wilaya kufanya kazi kwa bidii na weledi na waone kuwa uwepo wa ofisi hizo uwe chachu ya kuendelea kutoa taarifa za ukaguzi wa shule zenye ubora na kwa wakati. Ndalichako amewataka kuhakikisha kuwa changamoto zinazoainishwa katika kaguzi zao zinafanyiwa kazi ili kuinua ubora wa elimu hususan katika taaluma na sekta ya elimu kwa ujumla katika wilaya hizo.

"Tumieni ofisi hizi kuwa chachu ya kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa taarifa za changamoto zinazozikabili shule pamoja na sekta nzima ya elimu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka," amesema Profesa Ndalichako.

Prof. Ndalichako amesema serikali itahakikisha changamoto zote zinazowakabili wathibiti ubora wa shule nchini zinafanyiwa kazi kwa dhati ili kuzipunguza ama kuzimaliza kabisa ikiwemo ukosefu wa ofisi na vitendea kazi.

Akizungumzia uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu unaoendelea nchini, Profesa Ndalichako amesema suala hilo ni endelevu na litakuwa likifanyiwa kazi muda wote ili kuwezesha utoaji wa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.

Aidha, Waziri Ndalichako amewataka wathibiti ubora wa shule kwa kushirikiana na Maafisa Elimu kufanya tathimini za kina kila mara ili kubaini sababu halisi za mdondoko wa wanafunzi wote wa kike na kiume.

"Tumeona hapa Misungwi takwimu zinaonyesha mdondoko mkubwa zaidi upo kwa upande wa watoto, hivyo fanyeni tathimini ili tujue sababu na kuacha kuegemea upande mmoja wa mtoti wa kike na kwamba sababu ni mimba" amesema Profesa Ndalichako

Kurasa 1 ya 20

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…