Utekelezaji wa mradi utazingatia miongozo ya usalama wa mazingira na jamii. Hivyo, WyEST imeandaa vikao vya wadau kwa ajili ya kupokea maoni ya wadau ili kuboresha rasimu ya miongozo mitatu (3) iliyoandaliwa. Miongozo hiyo ni Mwongozo wa Usimamizi wa Usalama wa Mazingira na Jamii (Environmental and Social Management Framework – ESMF), Mwongozo wa Uhamishaji wa Makazi na Watu (Resettlement Policy Framework - RPF) na Mpango wa Ushirikishwaji wa Wadau (Stakeholders’ Engagement Plan –SEP).
Vikao vya kupokea maoni ya wadau vitafanyika mkoani Dar es Salaam, kuanzia saa 9:00 asubuhi kwa kulingana na jedwali lifuatalo.
Wadau | Ukumbi | Tarehe |
Taasisi zinazotekeleza Mradi wa HEET, Taasisi na wakala wa Serikali, Jumuiya za wataaluma vyuoni, Jumuisha za Wanafunzi Vyuoni, Jumuiya za wanafunzi wenye mahitaji maalumu | Maktaba UDSM | 13 Januari 2021 |
Asasi zisizo za Serikali, Mashirika, Makampuni, watu binafsi na wadau wa maendeleo | Maktaba UDSM | 14 Januari 2021 |
Kwa kuzingatia umuhimu wa miongozo hiyo, WyEST inawaalika wadau wote kufika na kutoa maoni yao kabla miongozo hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo kabla ya tarehe
15 Januari 2021:-
Miongozo hiyo pia inapatikana kupitia tovuti ya WyEST www.moe.go.tz