Lengo la Mradi ni kuongeza udahili katika vyuo vikuu vya serikali, kuongeza ubora wa mafunzo ili kuendana na soko la ajira kwenye programu za kipaumbele na kuboresha utendaji wa Serikali katika kusimamia Elimu ya Juu nchini.
Utekelezaji wa Mradi utazingatia Miongozo ya Usalama wa Mazingira na Jamii. Hivyo, WyEST imeandaa vikao vya wadau ambao ni: Taasisi zitakazotekeleza Mradi wa HEET, Taasisi na wakala wa Serikali, Jumuiya za wataaluma Taasisi za Elimu ya Juu, Jumuisha za Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu, Jumuiya za wanafunzi wenye mahitaji maalumu Taasisi za Elimu ya Juu, Asasi zisizo za Serikali, Mashirika, Makampuni, watu binafsi na wadau wa maendeleo; kwa ajili ya kupokea maoni ili kuboresha rasimu ya miongozo mitatu (3) iliyoandaliwa. Miongozo hiyo ni Mwongozo wa Usimamizi wa Usalama wa Mazingira na Jamii (Environmental and Social Management Framework – ESMF), Mwongozo wa Uhamishaji wa Makazi na Watu (Resettlement Policy Framework - RPF) na Mpango wa Ushirikishwaji wa Wadau (Stakeholders’ Engagement Plan –SEP).
Kwa kuzingatia umuhimu wa miongozo hiyo, WyEST inawaalika wadau wote kutoa maoni kabla miongozo hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine. Mwisho wa kupoke maoni ni tarehe 15 Januari 2020. Maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo: -
Aione: Tabitha Etutu
Miongozo hiyo inapatikana kupitia tovuti ya WyEST www.moe.go.tz
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabitha Etutu kwa Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. au Sakanda Gaima kwa Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona..