Jumanne, 03 Machi 2020 16:58

UZINDUZI WA KAMPENI YA KITAIFA YA KUSHIRIKISHA SKAUTI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka vijana nchini kubadili mtazamo wa jamii kuhusu rushwa kuwa ni sehemu ya utamaduni na mfumo wa maisha na kuwa rushwa ni adui wa wa haki.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Kushirikisha Skauti katika Mapambano dhidi ya Rushwa nchini iliyofanyika jijini Dodoma Profesa Ndalichako amesema kundi la vijana ni umuhimu wa kipekee katika kuleta mabadiliko ya kijamii hususan katika kubadili mtazamo wa jamii kuhusu utamaduni huo.

“kumekuwa na utamaduni uliojengeka kwa jamii ili upate mafanikio lazima utoe rushwa, wanafunzi ili wafanikiwe vizuri lazima watoe rushwa ya ngono imeendelea kushamiri hususan katika taasisi za elimu, vijana mnapaswa kusimama na kukemea ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mnapokutana na changamoto hizi” amesisitiza Ndalichako.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (MB) akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaamini kuwa ni wakati muafaka kwa vijana na watoto waliopo katika jamii, shule za msingi, sekondari na vyuo kuiishi kwa vitendo dhana ya kuzuia rushwa kwani ni adui wa maendeleo ya Taifa

Kapteni Mkuchika amesema Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa na utekelezaji wake unaonekana katika maeneo mengi mojawapo ikiwemo kuanzishwa kwa mahakama maalum ya kushughulikia kesi za rushwa na ufisadi.

Akizungumzia kuhusu Mkakati huo, Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza amesema unatarajia kutoa vijana milioni 16.3 kwenye shule za msingi na sekondari na kwamba endapo kila mmoja ataongea na watu wanne kuhusu masuala ya rushwa zaidi ya watanzania milioni 40 wataongea ubaya wa rushwa.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika uzinduzi huo amekipongeza chama cha Skauti kwa kuona umuhimu wa kushirikisha vijana katika kampeni ya kitaifa mapambano dhidi ya rushwa na kuwataka kutumia lugha rahisi ya Kiswahili katika kuwaelimisha vijana kuhusiana na masuala ya rushwa.

Read 1007 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…