Jumatano, 12 Februari 2020 04:02

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kujenga bwalo katika shule ya Mrisho Gambo iliyopo mkoani Arusha.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Wizara itajenga bwalo la chakula ili kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kuwa na sehemu nzuri na salama ya kupatia chakula watakapokuwa wakiishi katika mabweni yatakayojengwa na wizara.

"Nimeambiwa wanafunzi wa shule hii wanatoka maeneo ya mbali, Wizara ilishaahidi kujenga mabweni mawili sasa tutajenga na bwalo," amesema Dkt. Akwilapo.

Aidha, Dkt. Akwilapo amesema serikali ina wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika
mazingira salama na yenye miundombinu salama.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema shule hiyo imejengwa baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa Olasite baada shule yao kuzidiwa na wingi wa wanafunzi.

"Baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa hapa na kuona kweli kuna shida katika shule hii ya Olasite ndipo tukaanza kutafuta wadau mbalimbali ambao walijitokeza na kusaidia uanzishwaji wa ujenzi wa shule hiyo," amesema Gambo.

Mkuu wa shule hiyo, Fedelis Michael amesema mazingira ya wanafunzi kusoma mbali sana na shule ni changamoto kwao kwani njiani wanakutana na mambo mengi ambayo yanaweza kuwasababishia kushindwa kusoma vizuri.

Read 436 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…