Ijumaa, 04 Oktoba 2019 13:20

WAZIRI NDALICHAKO AWAASA WANAFUNZI WANAOMALIZA KIDATO CHA NNE KUWA NA MAADILI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema elimu bila nidhamu na maadili haiwezi kukusaidia kufanikiwa katika maisha.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 32 ya shule ya sekondari Suji iliyoko wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Amesema katika maisha ili mtu afanikiwe ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kazi aliyonayo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka na hata watu walio chini yako na kuwataka wanafunzi kuyaishi hayo mara baada ya kumaliza elimu ya kidato cha nne

Kiongozi huyo ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari Suji kwa kuwalea wanafunzi katika maadili mema ya kumjua Mungu na kuwapongeza kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya Kidato cha nne na cha sita.

Ndalichako amewataka wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo yao ili wengi zaidi waweze kufaulu kwa kupata daraja la kwanza.

"Pamoja na ufaulu wenu mzuri lakini nataka daraja la kwanza ziongezeke, kwa sababu ukiangalia matokeo ya shule hii kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2016 hadi 2018 hata kama hakuna daraja la nne lakini wanaopata daraja la kwanza ni wachache hivyo ongezeni juhudi ili ili huku kwenye daraja la kwanza muongezeke,"alisema Waziri Ndalichako

Amewataka wanafunzi kuwa na uzalendo na nchi yao ikiwa ni pamoja na kuzilinda tunu Taifa zilizoachwa na waasisi waxtaifa letu ambazo ni pamoja na amani, umoja na mshikamano

"Mnaona kazi kubwa ambayo Rais wetu wa Awamu ya Tano anaifanya anahakikisha rasilimali za nchi haziibiwi zinawanufaisha watu wote hivyo mnapomaliza mkamuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili dhamira yake ni kuona nchi yetu inapata maendeleo inafanikiwa ," alisema Waziri Ndalichako

Waziri Ndalichako ametumia fursa hiyo kuwatakia heri na mafanikio wanafunzi wote wa kidato cha nne wanaotarajia kuanza mitihani yao Mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Rozimary Staki amesema
Wilaya ya same ina shule za sekondari 53 ambapo 17 zinamilikiwa na watu binafsi pamoja na taasisi za dini.

Amesema kama Wilaya wamekuwa wakishirikia na na Viongozi wa Dini katika kuelimisha mabinti umuhimu wa kujitambua wanapokuwa shuleni.

Nae mkuu wa shule ya sekondari Suji Silnani Dismas amesema shule hiyo pamoja na kusisitiza masoma inawalea wanafunzi katika maadili na nidhamu ya hali ya juu kwa kuwa ni ya kanisa.

Dismas amesema shule hiyo ina wanafunzi takribani 568 na mafanikio wanayojivunia ni kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

Mwanafunzi bora katika masomo Tajiel Omary ambae anatarajia kuhitimu masomo ya kidato cha Nne mwaka huu amasema ufauli katika masomo unatokana na juhudi ambazo amekuwa akizifanya katika masomo ikiwa ni pamoja na kumuomba Mungu ili malengo yake yatimie.

Waziri Ndalichako pia alitembelea shule ya sekondari Makanya na kuongea na wanafunzi ambapo amewatakia pi heri katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne Mwezi Novemba mwaka huu.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
04/10/2019

Read 2540 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…