Alhamisi, 25 Julai 2019 02:04

NDALICHAKO: NIMERIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI WA SHULE ALIYOSOMA BABA WA TAIFA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa shule ya msingi ya Mwisenge na kuridhishwa na kasi ya ukarabati huo. Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati huo katika Shule aliyosoma Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Julius Nyerere, Waziri Ndalichako alisema ameridhishwa na kasi hiyo ya ujenzi huo ambao unahusisha ukarabati wa majengo ya kale, ukarabati wa madarasa, mabweni, ujenzi wa madarasa mapya, uzio wa shule, mnara pamoja na uboreshashi wa mazingira.

Mradi ambao unataraji kugharimu kiasi cha sh Milioni 706 ambazo zimetolewa na Wizara. “Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa mpaka sasa na viwango vya ujenzi wa madarasa na mabweni nao ni imara, kwani hata ujenzi wa ukuta unafanyika vizuri, kuta za mabweni ni mrefu na utawafanya watoto wakilala ndani wapate hewa vizuri” alisema Prof. Ndalichako. Kuhusu kusimama kwa ukarabati wa baadhi ya majengo ya kihistoria katika shule hiyo ambayo moja ya jengo linalengwa kuwa zahanati itakayotumika kwa ajili ya wanafunzi yaliyosimamishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Ofisi ya Mambo ya Kale, Waziri Ndalichako amewataka watalaam hao kufika mara moja ili kutoa muongozo unaohitajika kuwezesha kukamilisha ukarabati wa majengo hayo kwa wakati. “Ni vizuri ndugu zetu wa Mambo ya Kale wafike mara moja ili kutoa muongoza wa namna bora wa kufanya ukarabati wa majengo haya ya kihistoria yanapaswa kukarabatiwa kuwezesha walioyosimamisha ili ujenzi huo uweze kukamilika mapema kuwezesha wanafunzi kupata fursa ya kuyatumia, kwani kuendelea kukwamisha ama kuchelewesha ukarabati huo ni kuchelewesha maelekezo ya mhe rais.

Prof. Ndalichako amesema lengo la wizara ni kuona shule hiyo inakamilika mapema ili kutimiza maagizo aliyoyatoa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli ya kutaka shule hiyo ikarabatiwe iwe na hadhi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyesoma shuleni hapo. Na kutoa maelekezo ya shule hiyo kuwa na hadhi ya Baba wa Taifa na kukatua kero ya watu kuvamia shule hiyo kwa kujengwa ukuta Mapema MKuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Anney amemweleza waziri kuwa baadhi ya majengo hayajakamilika kutokana na kusimamishwa kwa ukarabati wa majengo hayo ya kihisitoria katika shule hiyo na Ofisi ya Mambo ya Kale yenye jukumu la kutoa muongozo wa namna gani ukarabati unapaswa kufanywa, ingawa toka kusimamishwa wataalam hao bado hawajafika kutoa maelekezo yeyote yale na tayari wameshawaandikia barua ya kuwakumbusha. “Lengo letu ni kuhakikisha ifikapo Oktaba 30 ukarabati huu uwe yamekamilika kabisa, lakini changamoto iliyopo sasa ni kukwama kwa ukarabati wa baadhi ya majengo ya kihistoria ambayo wenzetu wa mambo ya kale waliagiza ukarabati wake usimame mpaka watakapofika na kutoa maelekezo ya namna gani ufanyike lakini mpaka sasa hakuna mtaalam yeyote aliyefika pamoja na kuwaandikia barua, Amesema Dkt. Anney. Dkt. Anney ameishukuru wizara kwa kuipatia Wilaya ya Musoma fedha za kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea ikiwemo shilingi milioni 152 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za udhibiti ubora wa shule, ukarabati wa shule ya sekondari ya ufundi musoma ambayo imewekewa mitambo pamoja na vifaa vya kufundishia iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.2. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 24/07/2019

Read 1698 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…