Jumanne, 21 Mai 2019 14:29

TAARIFA KWA UMMA: JUU YA MAJENGO YA SHULE YA MSINGI MITAMBO

Baadhi ya majengo ya vyumba vya madarasa vilivyopo katika shule ya msingi Mitambo.

Kumekuwa na taarifa inayosambaa kwenye mtandao wa Instagram inayoonesha majengo ya Shule ya Msingi ya Mitambo iliyo Kata ya Madimba Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kutoa taarifa kwamba majengo hayo siyo yanayotumika katika Shule hiyo kwa sasa.

Shule hii ina usajili Namba EM14873 na ina madarasa ya kudumu ambayo yamejengwa na Serikali kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo na Halmashauri ya Wilaya husika. Kama ilivyo katika shule za maeneo mbalimbali nchini ujenzi wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo zaidi bado unaendelea na kwa kumbukumbu za Wizara, majengo hayo ya tope yaliyooneshwa katika Mtandao kwa sasa hayapo katika shule hiyo.

Picha halisi za madarasa katika shule hiyo ni kama zinavyoonekana hapo chini. Aidha picha hizo pia zinaweza kuonekana kwenye tovuti ya wizara www.moe.go.tz na mitandao ya kijamii ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwemo Instagram: wizara_elimutanzania twitter: wizara_elimuTz, www.wyestu.blogspot na www.facebook/moestvt.com.

Wizara imesikitishwa na taarifa hizi za upotoshaji na inatoa rai kwa watu wote kutambua umuhimu wa kuthibitisha ukweli wa taarifa anazokusudia kuzitoa kabla ya kuzisambaza.

Sylvia T. Lupembe

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Read 3170 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…