Kwa msingi wa maelezo hayo, wanafunzi wote ambao ni raia wa Tanzania, ambao wako nje ya nchi walikokwenda ama kwa Skolashipu zilizoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa ufadhili au uratibu wa Taasisi nyingine yoyote na wanajitambua kuwa taarifa zao hazifahamiki kwenye Ofisi za Balozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nchi wanakosoma, mnaelekezwa kuwasilisha taarifa zenu mapema katika Ofisi za Balozi zetu katika nchi mnazosoma.
Suala hili tunaomba mlipe uzito unaostahiki kwa kuwa litatusaidia wote kama nchi katika hali au matukio ya furaha na pengine wakati wa matatizo.
Tunasisitiza kuwa mtazingatia na kuona kuwa ni sehemu ya kutimiza wajibu mkiwa Watanzania.
Imetolewa na: