Jumatano, 08 Mai 2019 10:46

TAARIFA KWA UMMA: Wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebaini kwamba kuna wanafunzi ambao ni raia wa Tanzania wanaosoma katika Taasisi za Elimu ya Juu nje ya nchi lakini taarifa za uwepo wao katika nchi hizo hazifahamiki kwenye Ofisi za Balozi zetu katika nchi wanazosoma.

Kwa msingi wa maelezo hayo, wanafunzi wote ambao ni raia wa Tanzania, ambao wako nje ya nchi walikokwenda ama kwa Skolashipu zilizoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa ufadhili au uratibu wa Taasisi nyingine yoyote na wanajitambua kuwa taarifa zao hazifahamiki kwenye Ofisi za Balozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nchi wanakosoma, mnaelekezwa kuwasilisha taarifa zenu mapema katika Ofisi za Balozi zetu katika nchi mnazosoma.

Suala hili tunaomba mlipe uzito unaostahiki kwa kuwa litatusaidia wote kama nchi katika hali au matukio ya furaha na pengine wakati wa matatizo.

Tunasisitiza kuwa mtazingatia na kuona kuwa ni sehemu ya kutimiza wajibu mkiwa Watanzania.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Read 4103 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…