Jumamosi, 13 Aprili 2019 09:29

SERIKALI KUJENGA SEKONDARI NA CHUO CHA UFUNDI DODOMA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kujenga shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi katika jiji la Dodoma ili kutoa fursa za elimu kwa wakazi wa jiji hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mji wa kiserikali jijini Dodoma Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema shule hiyo ya sekondari itakayojengwa kwa Sh. Bilioni 13 itachukua wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.

Rais Magufuli ameongezea kuwa sh Bilioni 18 pia zitatumika kujenga Chuo kipya kikubwa cha ufundi kitakachotoa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali jijini Dodoma.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Dodoma kuhakikisha wanatumia vyema taasisi hizo za elimu katika kuwapatia maarifa vijana wao kwa maendeleo ya Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Rais Magufuli amezindua mji wa kiserikali katika eneo la Mtumba jijini Dodoma ambapo majengo hayo yatatumiwa wizara mbalimbali na baadhi ya Taasisi.

Imetolewa na

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

13/04/2019

Read 1685 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…