Ijumaa, 08 Machi 2019 15:08

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU KUFATILIA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leornald Akwilapo kufika katika shule ya Sekondari Kibaha kujionea jinsi kazi ya ukarabati ilivyo chini ya viwango ili achukue hatua zinazostahili.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika shule ya sekondari Kibaha kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo.

Kiongozi huyo amesema hajaridhishwa kazi inavyoendelea kwani hailingani na fedha ambayo tayari imeshalipwa na serikali tangu mwaka juzi walipokabidhiwa. Kazi hii ya ya ukarabati wa jingo la bweni na jingo la maabara ya fizikia katika shule hiyo inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA).

“Wakala huyu alipaswa kuwa amekamilisha ukarabati na ujenzi wa miundombinu jumla 31 katika shule hii, lakini mpaka sasa amekarabati majengo mawili tu na ukiyaangalia yako chini ya viwango huku akiwa ametumia zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 400.” Amesema Ole Nasha

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amewapongeza wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha kwa kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa bila kujali changamoto walizonazo za miundombinu ya mabweni, madarasa pamoja na vyoo.

“Wanafunzi hawa wanachukua mchepuo wa sayansi wanahitaji kujiongezea maarifa sasa nimeambiwa shule hii ina kompyuta nne tu hivyo namuagiza Katibu Mkuu alete kompyuta 50 shuleni hapa ziweze kuwasaidia wanafunzi” alisisitiza Naibu Waziri

Kwa upande wake Kaka Mkuu wa Shule hiyo Jonas Baraka amemweleza Naibu Waziri kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi za miundombinu kwani hata ile iliyokarabatiwa kwani vyoo havipitishi maji, ubovu wa vitasa vya milango pamoja na ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo ya shule.

Katika hatua nyingine Naibu Waziriameonyeshwa kutoridhishwa na matumizi ya  zaidi ya shilingili milioni mia moja  na hamsini ziliotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa  mabweni mawili katika sekondari ya Kwala na kumagiza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asumpter Mshama  kutuma  vyombo vya ulinzi na usalama kwenda kukagua mchakato mzima uliotumika katika ujenzi wa mabweni mawili ya shule hiyo.

Naibu Waziri Ole Nasha yupo katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule inayofadhiliwa na Wizara ya Elimu kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika Mkoa wa Pwani katika wilaya za Kibaha, Kisarawe na Rufiji.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
6/3/2019
Read 355 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…