Jumatano, 10 Oktoba 2018 14:24

WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WATANZANIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI

Watanzania wametakiwa kushikamana kwa kufanya Kazi kwa bidii kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na  Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili Taifa liweze kutumiza malengo ya  kufikia uchumi wa kati hadi ifikapo  mwaka 2025.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya 19 ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere linalofanyika katika chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri Ndalichako amesema Wizara itaendelea kukienzi Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kiendelee kuwa  Kitovu cha maadili katika kuwajenga Viongozi na vijana ikiwa ni pamoja  na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho  Prof. Shadrack Mwakalila amewataka viongozi na wanafunzi kuhakikisha wanakitumia chuo hicho kwa ufanisi ili kupata  mafunzo  yanayohusu uzalendo, uadiifu na kuwa mafunzo yanayotolewa  chuoni hapo ni yale ya muda mfupi na mrefu. 
Prof. Mwakalila amesema kila mwaka chuo hicho huandaa maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati wa Baba wa Taifa kwa Lengo la kujitathmini kama Taifa, tumetoka wapi na tuko wapi.
Katika kumbukizi hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa  ikiwemo ile inayohusu Uhuru na Maendeleo katika kuelekea uchumi wa Kati, umuhimu wa uzalendo na uadilifu, umuhimu wa misingi ya Azimio la Arusha katika kustawisha Viwanda vya ndani.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
10/10/2018

Read 180 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…