Jumanne, 09 Oktoba 2018 08:09

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA YATAKIWA KUTUMIA UTARATIBU WA FORCE AKAUNTI.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu Tanzania, (TEA) kuanza kutumia utaratibu wa Force Akaunti katika utekelezaji wa miradi ya Elimu wanayoisimamia kwa kuwa utaratibu huo unawezesha kazi kukamilika kwa wakati, lakini pia kujenga majengo yenye ubora kwa gharama nafuu.

Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akikagua shughuli za ujenzi katika shule ya Sekondari ya wasichana Nangwa na ile ya Endasak zilizopo Wilayani Hanang ambazo kwa pamoja ujenzi wake unatekelezwa na Wizara hiyo kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) na Mamlaka ya Elimu Tanzania.

“Nitawapeni mfano Shule ya Sekondari Endasak imejengewa bweni na Wizara ya Elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa zaidi ya shilingi milioni 170, huku miradi mingine inayotekelezwa na Wizara kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ikitumia kiasi hicho hicho kujenga mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja kwa utaratibu wa Force Akaunti,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo amesema mahitaji ya Taifa letu kwenye Sekta ya Elimu bado ni makubwa hivyo ni vizuri kurudi katika utaratibu wa kutumia Force Akaunti ili kuweza kuwapatia malazi wanafunzi wengi pamoja na kutatua changamoto nyingine zilizopo kwenye Sekta ya Elimu. 

Naibu Waziri huyo pia amewaagiza viongozi wa elimu mkoa wa Manyara kuhakikisha Shule ya Sekondari ya Endasak katika mwaka wa masomo 2019/20 inapangiwa wanafunzi wa kidato cha tano kwa kuwa tayari ina miundombinu inayotosheleza likiwemo bweni lililojengwa na Wizara hiyo.

Akizungunza na wanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya wasichana Nangwa na ile ya Endasak Mheshimiwa Ole Nasha amewataka wanafunzi hao kuwa na bidii katika masomo, waadilifu lakini pia kuwa wazalendo kwa nchi yao kwani kwa kufanya hivyo wataweza kuitetea nchi yao na kutoshiriki katika vitendo viovu.

Imetolewa na,

Kitengo cha MAwasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

09/10/2018

Read 145 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…