Jumatatu, 08 Oktoba 2018 11:38

OLE NASHA ATOA AGIZO KALI KWA VIONGOZI NA WAZAZI MKOANI MANYARA.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kote kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba, kwani kufanya hivyo kunawaondolea fursa ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.

Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwenda kwenye maeneo mengine kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, kumekuwa na tabia za kuwarubuni watoto hata wanapofaulu na kutakiwa kurejea kwa ajili ya masomo hawarejei, Katika hili pia wazazi msiwe sehemu ya kuchangia watoto wenu kwenda mjini kwa kuwa tu wanawatumia fedha kwa ajili ya matumizi bali hakikisheni mnawasimamia vyema na kuwapeleka shule pindi matokeo yanapotoka na kuonekana wamefaulu," alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.

Amewataka viongozi hao kutumia sheria kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule wanaandikishwa ili kutokuwa na wimbi kubwa la watoto wa mitaani wasiokwenda shule.

Awali Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Arnold Msuya alimweleza Naibu waziri huyo kuwa mkoa kwa sasa una mwamko mdogo wa Elimu hasa katika jamii ya wafugaji hali inayopelekea wazazi kutowaandikisha shule watoto wenye umri wa kuanza shule

Naibu waziri Ole Nasha pia ametembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi cha Mkoa Manyara na kuwataka kuboresha Mitaala yao ili mafunzo wanayoyatoa yaendane na wakati ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji ya soko la ajira ili kuongeza fursa ya vijana kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

8/10/2018

Read 123 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…