Ijumaa, 05 Oktoba 2018 15:05

NDALICHAKO AAGIZA KUONDOLEWA KWA MKUU WA CHUO CHA UALIMU SHINYANGA KWENYE NAFASI YAKE, ASEMA CHUO HICHO KINA HARUFU YA RUSHWA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kumuondoa mara moja Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Shinyanga Paschal Highmagway

kwenye nafasi yake kwa kushindwa kusimamia kazi za ujenzi lakini pia kumtetea Mkandarasi wa Affrique Enginearing and Construction Company Ltd ili hali Mkandarasi huyo ameshindwa kukamilisha kazi yake katika muda uliopangwa.

 

Waziri Ndalichako ametoa maagizo hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu chuoni hapo unaotekelezwa na wakandarasi wawili tofauti ambapo Mkandarasi mmoja ni Masasi Construction Company Ltd amekamisha kazi yake kwa asilimia 98 huku Affrique Enginearing and Construction Company Ltd ikishindwa kukamilisha kazi katika muda uliopangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ndalichako amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Diwani Athumani kuanza kuchunguza miradi inayotekelezwa katika chuo hicho pamoja na maafisa manunuzi wa Wizara ya Elimu kwa kuwa katika Chuo hicho kuna dalili za rushwa.

Waziri pia amemwelekeza Mkandarasi Afrique Enginearing and Construction Company Ltd kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika ndani ya mwezi mmoja na kuwa  tayari mkandarasi huyo  ameshalipwa kiasi cha bilioni 2 na milioni 700. 

“Haipendezi viongozi wa umma kila siku kukemea watendaji, kutumbuana kila tunapokutana kwenye majukumu, tunatakiwa tunapokutana tuwe tunakaa na kufurahi lakini kwa mtindo huu wa kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati serikali haitamvumilia mtu.

Profesa Ndalichako amesema kuwa fedha inayotolewa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule ya vyuo ni sumu na endapo itatumika vibaya waliohusika wataitapika fedha hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amemhakikishia Waziri kuwa Uongozi wa Wilaya utasimamia kwa karibu kuhakikisha maelekezo aliyoyatoa yanatekelezwa lakini pia amewataka wakandarasi wababaishaji wabadilike na wasipobadilika basi uongozi wa Wilaya utawabadilisha.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
5/10/2018
 
Read 225 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…