Alhamisi, 09 Agosti 2018 07:48

WAZIRI NDALICHAKO AIAGIZA NACTE KUFUNGIA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO KWA UBABAISHAJI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuendelea kufungia vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ubabaishaji ili kulinda ubora wa Elimu na Ujuzi kwa wanafunzi.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akizindua Baraza la Uongozi la Taifa la Elimu ya Ufundi ambapo amewataka NACTE kufungia hata vyuo vya serikali kama itabainika kutoa mafunzo yasiyo na ubora.

“Hatutaki kuwa na utitiri wa vyuo vingi ni bora kuwa na vichache lakini vitoe wahitimu wenye ujuzi na maarifa ambao wanaweza kuwa na mchango katika Taifa letu.” Amesisitiza Waziri Nalichako.

Pia Waziri Ndalichako amekagua Maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi inayojengwa Majimatitu Wilayani Temeke yenye lengo la kupunguza mlundikano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Majimatitu A yenye wanafunzi zaidi ya 7000.

Imetolewa na :

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

9/8/2018

Read 5915 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…