Jumatano, 08 Agosti 2018 08:35

WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI MAAFISA WATATU WA WIZARA YA ELIMU.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo kumsimamisha kazi Afisa manunuzi Audifasy Myonga na watumishi wengine wawil wa Chuo cha Ualimu Morogoro.
Waziri Ndalichako ametoa maagizo hayo mkoani Morogoro baada ya kutembelea chuo Cha Ualimu Morogoro na kukuta idadi kubwa ya vifaa vya maabara visivyotumika huku muda wa matumizi ya vifaa hivyo ukikaribia kuisha muda wake wa matumizi.
Ndalichako amesema ununuzi wa vifaa hivyo unaonyesha kuwa na shaka kwani vifaa hivyo vilinunuliwa kwa awamu mbili ndani ya mwezi mmoja huku gharama ya manunuzi ikionyesha kupanda mara mbili hadi tatu kutoka gharama ya awali.
“Mkuu wa Chuo ameeleza vizuri kabisa kuwa vifaa hivyo vilinunuliwa bila wao kushirikishwa, sasa unajiuliza mnunuzi amewezeje kununua vifaa vya maabara bila kuwashirikisha watumiaji,” alihoji Waziri Ndalichako .
Pia, Waziri Ndalichako ametembelea shule ya Sekondari ya Mzumbe kwa lengo la kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo unaofanywa na wizara ambapo amewataka walimu na wanafunzi kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo yao ili wafaulu kwa viwango vya juu.
Imetolewa na :
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
8/8/2018

Read 5969 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…