Jumanne, 07 Agosti 2018 08:29

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Bodi mpya ya Huduma za Maktaba Tanzania kuhakikisha inaanzisha Maktaba za Wilaya ili kuwawezesha watanzania wengi kunufaika na Elimu na Maarifa yatokanayo na usomaji wa vitabu.
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi hiyo na kusisitiza kuwa kuwepo kwa maktaba hizo kutaondoa changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata maktaba za mikoa.
“Wananchi wanapenda kusoma vitabu sasa natoa rai kwenu Bodi mpya mshirikiane na Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa kuanzisha Maktaba katika Wilaya zote, sisi kama Serikali tutaendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha tunaimarisha utoaji wa huduma za maktaba nchini.” Alisisitiza Ndalichako.
Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ametemblea Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kuzindua Baraza la Usimamizi la Taasisi hiyo ambapo amelitaka baraza hilo kuboresha vigezo vinavyotumika kusajili vituo vinavyotoa Elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi pamoja na kusimamia ubora wa elimu inayotolewa.
Imetolewa na :
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
7/8/2018

Read 5770 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…