Jumatatu, 06 Agosti 2018 08:10

AWAMU YA PILI MAFUNZO UTHIBITI UBORA YAANZA KATIKA KANDA TANO

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza awamu ya pili ya kutoa mafunzo kwa Wathibiti Ubora wa shule kwa Kanda za Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Morogoro na Mtwara juu ya kutekeleza mfumo mpya wa Uthibiti ubora wa shule.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya wathibiti ubora mkoani Arusha Naibu Waziri William Ole Nasha amewataka watumishi hao kusimamia mfumo na mxhakato wa utoaji wa Elimu kwa kuhakikisha Sera, kanuni , sheria na mongozo inazingatiwa na wadau wote katika sekta ya Elimu.

Naibu waziri ole Nasha amewataka wathibiti ubora kuhakikisha dhamira ya serikali inatimizwa kwa wathibiti ubora wa shule kuhama kutoka katika dhana ya ukaguzi kama wajuaji zaidi, au polisi kwa kukagua zaidi na badala yake wawe wathibiti ubora wa shule kwa kuhakikisha kuwa wanawasaidia walimu, kwa lengo la kuhakikisha serikali inafikia malengo ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa wizara hiyo, Euphrasia Buchuma amefungua mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Wathibiti Ubora kuzingati mafunzo yanayotolewa ili kuwawezesha kufanyia kazi yale yote yanayoelekezwa.

Buchuma amesema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wathibiti ubora wa shule kuweza kufanya ukaguzi wa shule kwa kutumia mfumo mpya ambao ni shirikishi unaoangalia zaidi tendo la kujifunza, kufundisha na kufanya upimaji katika ngazi ya darasa.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo mthibiti ubora wa shule kutoka Manispaa ya Ilala Diana Justine amesema mafunzo hayo yatawawezesha kutatua changamoto wanazokuta nazo shuleni kwa kushirikiana na walimu, wanafunzi na jamii tofauti na awali walipokuwa wanakwenda kuangalia matatizo bila kutoa suluhisho la matatizo hayo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

6/8/2018

Read 5954 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…