Jumapili, 05 Agosti 2018 09:37

NDALICHAKO ATAKA SHULE YA SEKONDARI MANGA DELTA KUPANDISHA TAALUMA

Waziri wa Elimu, Sayamsi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka walimu wa shule ya sekondari Manga Delta iliyoko wilayani Kibiti mkoani Pwani kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi kimasomo ili taaluma katika shule hiyo iweze kupanda.

Waziri Ndalichako ametoa agiza hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule hiyo ambapo amesema hajaridhishwa na mwenendo wa taaluma katika shule hiyo.

Amesema pamoja na serikali kuwekeza fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo bado imekuwa ikishuka kitaaluma mwaka hadi mwaka.

“Serikali imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 256 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa na bweni juhudi hizi ziende sambamba na ufundishaji ili taaluma ipande” Alisisitiza Ndalichako

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano kila mwezi imekuwa ikitoa kiasi cha silingi bilioni 20. 8 kugharamia Elimu bila malipo pamoja na kutoa shilingi laki mbili na nusu za posho ya madaraka kwa Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata hivyo amewataka kuwajibika ili kupandisha taaluma ya shule hiyo.

Waziri wa Elimu amehitimisha ziara yake ya siku mbili ya kikazi wilayani Kibiti mkoni Pwani kwa kukabidhi gari ya Idara ya Udhibiti Ubora kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo pamoja na pikipiki kumi na sita kwa Waratibu Elimu Kata.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

5/8/2018

Read 5779 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…