Ijumaa, 06 Julai 2018 23:09

DK. SEMAKAFU ASEMA HAKUNA ATAKAESALIMIKA MATUMIZI YA FORCE AKAUNTI

Serikali imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakayekiuka utaratibu wa kutumia Force Akaunti katika kutekeleza shughuli za ujenzi na ukarabati kwenye Vyuo vya Maendeleo ya wananchi (FDC’S).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Dk. Avemaria Semakafu mjini Morogoro wakati wa akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wakuu wa vyuo, maboharia na wahasibu kuhusu utaratibu wa kutumia Force Akaunti katika shughuli za ujenzi na ukarabati katika vyuo vya FDCs.

Alisema utaratibu huo ukokisheria na kwamba mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha kupata taaluma ya kutumia utaratibu huo ambapo amewataka washiriki hao kwenda kutumia taaluma hiyo kama nyenzo kuleta mabadiliko wakati wa kutekeleza miradi katika maeneo yao.

“Ni muhimu kwa Wakuu wa Vyuo na wote mtakaohusika katika shughuli za ujenzi na ukarabati kuhakikisha mnafuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa kuwa hakuna atakaesalimika kwa kuvunja sheria hizi,” alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo Dk. Semakafu.

Amesema Vyuo vya maendeleo ya Wananchi vilianzishwa kwa malengo mahususi ikiwa nipamoja na kutoa stadi na mafunzo kwa wananchi hivyo miradi hiyo ikikamilika kwa wakati vyuo vitaweza kutimiza malengo yake lakini pia thamani halisi ya matumizi ya fedha (Value for Money) zaujenzi na ukarabati zitaonekana.

Mafunzo hayo ya utaratibu wa kutumia Force Akaunti yameshirikisha wajumbe kutoka Vyuo vya maenedeleo ya wananchi 11 na yameendeshwa na Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Ajira (ESPJ).

Imetolewana;

Kitengo cha Mawasiliano,

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

06/07/2018                

Read 2538 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…