Jumatano, 04 Julai 2018 07:45

WAZIRI NDALICHAKO AIELEKEZA COSTECH KUPELEKEA MIONGOZO YA KUSAIDIA WABUNIFU KWENYE HALMASHAURI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce NDALICHAKO ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia, COSTECH -kuhakikisha miongozo yote ya namna yakuwasaidia wabunifu inapelekwa katika ngazi ya Halmashauri ili kuwezesha kupatikana kwa bunifu zitakazosaidia nchi kufikia uchumi wa viwanda.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo katika kongamano la sita la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu linalofanyika jijini Dar es Salaam.

Ndalichako amesema miongozo ikipelekwa kwenye halmashauri itasaidia kupatikana kwa wabunifu watakaoendeleza Teknolojia na kufanya kazi katika viwanda.

Waziri huyo mwenye dhamana ya kusimamia Elimu, Sayansi na Teknlojia amesema uchumi wa viwanda unategemea Sayansi na wataalamu wenye ujuzi wakutengeneza na kubuni bidhaa mbalimbali zitakazotumika   viwandani lakini pia kuiletea jamii Maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH Dkt. Amos Nungu, amesema Kongamano hilo la siku tatu Lina lengo la kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kuendeleza viwanda.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

4/7/2018.

Read 2247 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…