Jumatano, 04 Julai 2018 05:36

SERIKALI IMEKABIDHI PIKIPIKI ZAIDI YA 2500 KUBORESHA ELIMU NCHINI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Leo imekabidhi Pikipiki zaidi ya 2500 kwa Waratibu Elimu Kata ili ziwasidie katika kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuimarisha Elimu hapa nchini.

Pikipiki hizo zinakabidhiwa Leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ambapo amesema Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (LANES) umenunua Pikipiki hizo 2894 kwa zaidi ya shilingi bilioni Nane.

Waziri Ndalichako amesema pikipiki hizo zitasambazwa nchi nzima kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI.

"Rais alipoingia madarakani alihaidi kuimarisha ubora wa Elimu, sasa moja ya mikakati ya kutekelez hilo ndiyo maana hii Leo tunashuhudia vitendea Kazi hivi ambavyo vitasambazwa nchi nzima, lengo hapa ni kuhakikisha Elimu inayotolewa inakuwa bora na kuhakikisha nchi inakuwa na matokeo chanya kiuchumi” amesema Ndalichako.

Waziri Ndalichako pia amewataka waratibu elimu Kata hao kuhakikisha pikipiki hizo zinatumika kwa ajili yakusimamia elimu katika maeneo yao na kupandisha ufaulu na si vinginevyo.

Kwa upande wake Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewataka waratibu elimu kata kuhakikisha wanasimamia taaluma katika maeneo yao.

Aidha, Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Mikoa, Halmashauri, Manispaa na Majiji kuweka utaratibu wa kuzihudumia pikipiki hizo katika maeneo yao.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

3/7/2018.

Read 2009 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…