Jumatano, 04 Julai 2018 04:40

NAIBU WAZIRI OLE NASHA: VYUO VYA UFUNDI VINAMUANDAA KIJANA KUJIAJIRI NA KUAJIRIWA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka vijana kuachana na dhana ya kuwa ili kufanikiwa katika maisha lazima uwe umesoma hadi chuo Kikuu lakini ukweli ni kuwa vyuo vya ufundi vinamuandaa kijana kuwa na uwezo wa kujiajiri na pia kuajiriwa ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo wakati alipotembelea Baadhi ya Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo ambazo zinashiriki maonesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Ole Nasha amewahakikishia Watanzania kuwa Elimu inayotolewa hapa nchini ina viwango vya ubora unaokubalija na ndiyo maana vijana wengi wanaajiriwa nje ya nchi kutokana na kile wanachokuwa wamekisomea.

Naibu Waziri ameleza kuwa serikali ya awamu ya Tano imeboresha Mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya Ufundi kwa kununua mitambo na vifaa vya kisasa ili kuimarisha mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo.

“ Uwekezaji huu mkubwa unalenga kuhakikisha vijana wanaohitimu katika vyuo vya Ufundi nchini wanakidhi soko la ajira la ndani na nje y nchi,”amesema Mheshimiwa Ole Nasha.

Taasisi zinazoshiriki Mamlaka ya Ufundi stadi- VETA, CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Cha Mzumbe, Taasisi ya Teknolojia-DIT, Baraza la Ufundi la Taifa-NACTE, Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS na Tume ya nguvu za Atomiki.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

3/7/2018.

Read 1846 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…