Jumatano, 06 Juni 2018 12:08

WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI KUAGA NA KUZIKA MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONSOLATA • AWATAKA WATANZANIA KUISHI KWA KUPENDANA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amewataka watanzania kujenga tabia ya kupendana, kuvumilia na kuhurumiana katika maisha ya kila siku.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo mkoani Iringa mara baada ya kuongoza mamia ya wananchi wakati wa ibada ya kuaga miili ya mapacha walioungana Maria na Cosolata katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha RUAHA mkoani Iringa.  

Amesema Maria na Consolata katika uhai wao waliishi wakiwa wameungana kwa hiyo waliishi kwa kuvumiliana na kupendana pia.

Amesema, Watanzania wanatakiwa kujiuliza kwa nini Maria na Consolata wamezaliwa Tanzania na Siyo nchi nyingine? amesisitiza kuwa watoto hao wamezaliwa nchini hapa ili iwe funzo kwa watanzania.

Maria na Consolata watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.

Maria na Consolata Mwakikuti walifariki jumamosi saa mbili usiku Juni 2 mwaka huu na miili yao itapumzishwa kwenye nyumba yao ya milele kwenye makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki Tosamaganga mkoani Iringa.

Kwa upande wake sista Calista Ludega ambaye ni Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Theresa wa Mtoto wa Yesu Jimbo Katoliki la Iringa amesema kuwa wamewazika Maria na Consolata mahala wanapolala Masista wa Maria Consolata kwa ajili ya kuwaenzi masista wa Wamishionari wa Consolata kwa kuwa wao wamekuwa sehemu kubwa ya malezi tangu waliopozaliwa watoto hao hadi wanapomaliza maisha yao duniani.

Familia ya Baba na mama wa mapacha hao kutoka Mkoani Mbeya na Kagera, masista wa Consolata wa Iringa na waombolezaji wengine wameungana katika kuwasindikiza katika safari yao ya mwisho duniani

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

06/06/2018

Read 752 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…