TANZANIA YAISHUKURU BENKI YA DUNIA KWA KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA ELIMU

Published on Monday 07 June, 2021 23:24:29

Serikali ya Tanzania imeishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuchangia katika kufadhili Miradi ya Elimu inayowezesha kuongeza ubora wa elimu, kuongeza nafasi na kuleta usawa katika upatikanaji wake.

Hayo yamesemwa leo Juni 7, 2021 Jijini Dodoma  na Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, katika kikao kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dkt Taufila Nyamadzabo ambapo amesema miradi hiyo pia inasaidia kuimarisha miundombinu ya kufundsha na kujifunzia katika ngazi zote za elimu nchini nakuahidi kusimamia utekelezaji wake kwa wakati na kwa mafanikio.

Katika kikao hicho  kilichohudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu  wamezungumzia utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Nchini.

Waziri Ndalichako ameongelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kuwa ni  , Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambao umesaidia sana utekelezaji wa Sera ya Elimu bila malipo ambapo kupitia mradi huo serikali imeongeza madarasa katika maeneo yenye wanafunzi wengi, matundu ya vyoo, mabwalo, mabweni ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya na kukarabati shule kongwe.

Ndalichako pia amezungumzia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambao unatekelezwa kwa dola za kimarekani milioni 500 na una lengo la kuimarisha elimu ya sekondari kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto wa kike na wa kiume. Mradi huu utawezesha ujenzi wa shule mpya 1000 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kila moja, ukarabati na upanuzi wa shule kongwe 50 ili kuongeza nafas zaidi za kidato cha tano na sita. Mradi huu pia utaongeaza nafasi kwa watoto kike kwa kujenga shule mpya za wasichana 26 moja kwa kila mkoa  zitakazo chukua wanafunzi 1500 kila mmoja.

, “ kwa mradi huu tuko tayari kabisa katika kutekeleza hasa eneo la kuongeza nafasi za masomo kwa kujenga shule ambazo zitakuwa karibu na maeneo wanayoishi wanafunzi, hii ni pamoja na zile shule 26 za wasichana na uborshaji vituo kwa aliji ya kutoa elimu kwa njia mbadala ambayo imesaidia wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali kuendelea kusoma na kuweza kufanya mitihani kurejea katika mfumo rasmi, hivyo nikuhakikishie tutatekekeza kwa ubora na kwa wakati”

Ametaja mradi mwingine unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kuwa ni Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) unaotekelezwa kwa Dola za Kimareni milioni 425. Amesema Mradi huo utasaidia kuongeza miundombinu ya elimu ya juu, kuongeza udahili kwa takribani asilimia 30, kutoa nafasi ya masomo kwa Wahadhiri 600 katika ngazi ya Uzamivu (PhD), pia itatoa nafasi kwa Wahadhiri kufanya tafiti na kuongeza machapisho. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu  amemuhakikishia Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dkt. Taufila Nyamadzabo kuwa fedha za  miradi ya elimu zitazopokelewa kutoka Benki ya Dunia  zinatumika vizuri ili kufikia malengo yaliyowekwa. Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo pia kusisitiza juu ya umuhimu wa kuboresha na kuongeza nafasi za elimu ya awali nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dkt. Taufila Nyamadzabo amesema kwa Nchi yoyote kuendelea inahitaji nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ambayo inaanza kuandaliwa kuanzia katika ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari na elimu ya juu, hivyo ni muhimu kuhakikisha fedha zinatengwa na kutumika kama zilivyokusudiwa ili kufikia malengo. 

Read 408 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top