Ministry of Education and Vocational Training

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2012 | Print |
MABADILIKO YA SHULE NA MACHAGUO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA 5 MWAKA 2012

Tarehe 27/03/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2011. Katika tangazo hilo Wizara iliwahimiza wanafunzi kuripoti katika shule zao walizopangwa kabla ya tarehe 12/04/2012. Baada ya tangazo hilo, Wizara imepokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara imetafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/machaguo kwa wanafunzi wenye sababu zifuatazo:
§       Waliopangwa shule za kutwa mahali ambapo hawana pa kuishi;
§       Waliopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
§       Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
§       Walioomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
§       Walioomba kubadili ‘combinations’ ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali

Wakuu wa shule wanaelekezwa kuwapokea wanafunzi hawa katika shule hizo mpya na kuwasiliana na wakuu wa shule walizopangwa awali wawatumie ‘Sel form’ za wanafunzi hawa. Aidha, mnatakiwa kuhakiki uhalali wa kila mwanafunzi mnayempokea kwa kutumia orodha ya majina yaliyomo katika tovuti pamoja na Result Slip za wanafunzi hao.

Wizara inawaagiza wanafunzi wote waliokubaliwa kubadilishiwa shule/combinations ambao taarifa zao zipo kwenye tovuti waripoti mara moja katika shule hizo. Wizara haitatoa barua kwa mwanafunzi yeyote. Aidha kuanzia sasa Wizara haitapokea maombi yoyote ya kubadilisha shule/combinations. Endapo yatakuwepo maombi yo yote yafuate utaratibu wa kawaida wa uhamisho kupitia kwa wakuu wa shule.

Imetolewa na
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
icon ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE-MACHAGUO-2012 (262.76 kB) 
 

Search School

You are here  : Home