Jumatatu, 20 Machi 2017 13:38

RAIS WA BENKI YA DUNIA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI ZANAKI.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifurahia jambo na mgeni wake  Dkt. Jim Yong Kim ambaye ametembelea shule ya msingi zanaki iliyopo jijini Dar es salaam hii leo. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifurahia jambo na mgeni wake Dkt. Jim Yong Kim ambaye ametembelea shule ya msingi zanaki iliyopo jijini Dar es salaam hii leo.

Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim  leo ametembelea Shule ya msingi zanaki na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika nyanja ya Elimu, huku akiwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kuja kuwa viongozi wenye maadili hapo baadae.

Dkt. Kim amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya hiyo  iliyopo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amewataka viongozi wenye mamlaka na sekta ya ELIMU kuendelea kuwajibika na kuwekeza zaidi katika Elimu.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema benki ya Dunia ni taasisi ambayo imekuwa ikifadhili ujenzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini na kuwa hivi sasa wizara inafanya mazungumzo ili benki hiyo  ifadhili Elimu maalumu, pamoja na kupata vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia.

Read 935 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…