Jumanne, 10 Aprili 2018 04:55

UJENZI CHUO CHA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI CHA MKOA WA KAGERA KUANZA OKTOBA 2018

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodutus Kinawiro amesema tayari Serikali imekamilisha ujenzi wa Miundombinu muhimu ya barabara na umeme katika Kijiji cha Burugo ambapo Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi cha Mkoa wa Kagera kinatarajiwa kujengwa.

Kinawiro amesema hivi sasa Mkoa upo katika kukamilisha miundombinu ya maji na kuwa tayari suala hilo limewekwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19.

Kukamilika kwa Miundombinu hiyo kunatoa fursa ya kuanza kwa ujenzi wa chuo hicho ambapo Ujumbe wa timu ya Wataalam kutoka Kampuni ya ujenzi ya Kichina (CHINA QIYUAN ENGINEERING CORPORATION) inayotarajiwa kusimamia ujenzi wa Chuo hicho umetembelea eneo hilo ambapo umekiri kuridhishwa na hatua hizo ambazo serikali imezitekeleza.

Kwa upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa Kampuni hiyo Fang Kefeng amesema uwepo wa barabara, umeme na maji katika eneo la mradi utawawezesha kutekeleza ujenzi bila kikwazo na kuwa tayari wameandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kwamba mradi utaanza mara baada Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuridhia michoro iliyoandaliwa kwa ajili ya Chuo hicho.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Enock Kayani amesema Mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba Mwaka huu mara baada ya Kampuni hiyo kufanya maboresho yaliyotolewa na Wizara katika michoro yao na kwamba mradi mzima utagharimu fedha za Kitanzania takribani bilioni 22 na utafanyika kwa awamu mbili .

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,                                                                                       

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

9/04/2018

Read 50826 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…