Ijumaa, 06 Aprili 2018 12:08

DK SEMAKAFU AZUNGUMZIA HAKI ZA MTOTO

Serikali ya awamu ya Tano imesema katika kulinda haki za mtoto imedhamiria kujenga shule za Elimu Jumuishi na zile za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika kila mkoa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave maria Semakafu jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa wadau unaojadili haki za mtoto.

Dk. Semakafu amesema lengo la ujenzi wa shule hizo ni kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wapata Elimu bila vikwazo vya aina yoyote kwani Elimu ni msingi wa Maenedeleo.

Amesema katika kutekeleza hilo tayari Wizara hiyo inajenga shule ya mfano kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika chuo cha Ualimu Patandi kilichopo mkoani Arusha, ambapo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa shule ya msingi mpaka Sekondari.

Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wote wenye umri wa kwenda shule bila kuangalia changamoto za kimaumbele walizonazo watoto wao kwa kuwa tayari Serikali imewekeza katika eneo hilo.

Mwakilishi wa UNICEF katika masuala ya Elimu nchini Tanzania Cecilia Baldeh amesema tayari Tanzania imekwisha piga hatua katika kulinda na kutetea haki za mtoto ikiwa ni pamoja na Serikali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda kwa kuwa Elimu msingi hivi sasa inatolewa bure.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

6/04/2018

Read 59071 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…