Ijumaa, 09 Machi 2018 09:20

NAIBU WAZIRI AFUNGA MAFUNZO.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amewataka watumishi wapya wa Wizara hiyo kuwa waadilifu

 katika utendaji kazi pamoja na kutunza siri katika maeneo wanayofanyia kazi.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa rai hiyo mjini Dodoma wakati akifunga mafunzo kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo, mafunzo ambayo yamelenga kuwakumbusha taratibu, sheria na miongozo ya kazi inayotakiwa  katika utumishi wa Umma.

Naibu Waziri huyo amesema anaamini mafunzo yaliyotolewa yatawawezesha kuwa watumishi bora wa umma  ambao wanafahamu vema mipaka ya kazi, taratibu za kiutumishi, lakinipia haki na wajibu katika utendajikazi.

Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri Ole Nasha amemuagiza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo Moshi Kabengwe kuandaa utaratibu wa mafunzo kwa watumishi wengine wa Wizara hiyo  ili kuwakumbushia taratibu, kanuni na miongozo  ili kuepuka ukiukaji wa maadili na pia Kuleta Chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi miongoni mwa watumishi.

Nae mmoja wa watumishi aliyeshiriki mafunzo hayo Lazaro Julius  kutoka Ofisi ya Kamishna  wa Elimu wa Wizara hiyo amesema mafunzo hayo ni muongozo thabiti katika kutekeleza majukumu ya kazi za kila siku katika utumishi wa Umma,ambapo ameahidi kuzingatia na kutekeleza yote aliyoelekezwa.

Mafunzo kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo yamefanyika kwa siku nne kuanzia Machi 6, 2018 na yameshirikisha waajiriwa wapya kutoka Wizara ya Elimu Makao Makuu, na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo.

Imetolewa na;

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
9/3/2018
Read 122128 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…