Ijumaa, 09 Machi 2018 10:51

OLE NASHA APIGA MARUFUKU WANAFUNZI WA SHULE KUNYIMWA VYETI KWA KUTOKAMILISHA MICHANGO.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amepiga Marufuku Wanafunzi kunyimwa vyeti pindi wanapomaliza

shule kwa madai ya kutokamilisha michango pindi walipokuwa wanasoma.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Tabora alipokutana na Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari kuzungumzia namna ambavyo wanapaswa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John PombeMagufuli la kukataza michango shuleni kwa kuwa Serikali inagharamia ElimuMsingi.

Naibu Waziri huyo amesema Magufuli hajakataza uchangiaji wahiari isipokuwa amekataza michango holela ambayo ilikuwa ikichangishwa bila utaratibu na kumzuia Mwanafunzi kuendelea na masomo kwa madai kuwa hajachanga mchango wa aina fulani.

‘Waraka wa Elimu Namba 6 wa mwaka 2016 unaeleza wazi namna Elimu bila malipo itakavyotekelezwa na nijukumu la mzazi kwa mtoto wake hivyo ni marufuku Mwanafunzi kubakizwa nyumbani au kutopewa cheti chake anapomaliza Shule kwa madai kuwa hajakamilisha mchango fulani’.amesema Ole Nasha

Pia ametoa rai kwa walimu wote nchini kujielekeza kwenye jukumu lao la msingi la kufundisha badala ya kujihusisha na uchangishaji wa mchango wa aina yoyote na kwamba michango yote ya hiari itaratibiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri husika kupitia watendaji wake.

Imetolewana:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

09/03/2018

Read 119747 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…