Ijumaa, 09 Machi 2018 16:47

NDALICHAKO AWATAKA WANAWAKE KUFANYA KAZI KWA BIDII.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka Wanawake nchini kuendelea kufanya kazi kwa

bidii ili kuonyesha Thamani ya Mwanamke katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Waziri Ndalichako amesema bidii pekee katika shughuli mbalimbali za kujiletea Maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ndiyo itaonyesha mchango wa Mwanamke na kumfanya athaminiwe na kumuwezesha kupata nafasi kubwa na nzuri zaidi za kutumikia Taifa ikiwa ni pamoja na kufuta dhana potofu ya kuwa Mwanamke hawezi.

Waziri Ndalichako amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya Akademia ya Sayansi Tanzania walati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ili kujadili mchango wa Mwanamke katika kuleta Maendeleo Endelevu ambalo limeshirikisha Wanawake na Wadau wengine kutoka nchi mbalimbali.

Kwa upande wake Spika Mstaafu Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuhakikisha wanapata Elimu ambayo itawawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwa na uthubutu wa kufanya shughuli ambazo wanaamini watazifanya kwa umakini ili kuonyesha uwezo walionao katika jamii inayowazunguka.

Imetolewana:

Kitengo cha Mawasilino Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

8/3/2018

Read 99656 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…