Alhamisi, 08 Machi 2018 03:58

MLOGANZILA YAPOKEA MSAADA WA DAWA.

Serikali ya Korea leo imeikabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Moja kwa Serikali ya Tanzania

ikiwa ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jijini Dar es Salaam ili zitumike katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila.

Mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ndalichako ameishukuru Serikali ya Korea kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kutumia vema miundombinu ya Chuo kwa kujifunzia na kufundishia ili kujijenga kitaaluma kwalengo la kumaliza tatizo la uhaba wa Madaktari na Wataalam wa Afya hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya dawa hizo Kiongozi wa Ujumbe wa Korea wa Kamati ya Afya na Huduma za Jamii ya Bunge la nchi hiyo, Jun Hey Sook amesema msaada huo wa dawa ni ushirikiano katika kuboresha sekta ya Afya.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Read 51654 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…