Jumatano, 21 Februari 2018 10:05

TAARIFA KWA UMMA: TAARIFA INAYOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Kumekuwa na Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha makisio ya gharama ya mazishi ya Akwilina Bafhata Akwilini aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuufahamisha Umma kuwa Bajeti hiyo inayosambaa kwenye mitandao ni makadirio yaliyoandaliwa na familia ya Marehemu.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dkt. Leonard Akwilapo, imepokea makisio ya gharama za mazishi kiasi cha Shilingi 80,150,000/= kutoka kwa Msemaji wa Familia hiyo Bw. Festo Kavishe.

Baada ya kupokea makisio hayo Katibu Mkuu Dk. Akwilapo alitahadharisha kuwa kuna baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwa kuwa kisheria hayagharamiwi na Serikali. Pia katika makisio hayo kuna gharama ambazo zilikuwa zimepewa makadirio ya juu.

Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu aliagiza kuwe na kikao kati ya Wizara na ndugu wa marehemu ili kuweka sawa changamoto hizo ili kuwa na bajeti ya pamoja, ambapo kikao hicho kilifanyika jana jioni na kufikia muafaka.

Hivyo Wizara inapenda kuufahamisha Umma kuwa taratibu nyingine za maandalizi ya mazishi zinaendelea vizuri.

Imetolewa na:

    Mwasu Sware

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

21/2/2018

Read 66427 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…