Jumamosi, 03 Februari 2018 10:43

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA BODI YA USHAURI YA ADEM NA KUITAKA BODI HIYO IFANYE KAZI KWA WELEDI.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekolojia Profesa Joyce Ndalichako  leo amezindua bodi ya ushauri ya wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) ambapo ameitaka bodi  hiyo

iisaidie ADEM kutimiza majukumu yake ipasavyo  kwa upande wa kutoa mafunzo, nidhamu ya utendaji kazi na kusimamia vyema matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya Taasisi hiyo.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo hii leo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza kuwa anategemea kuona matokeo chanya kutoka kwenye bodi hiyo kwa kuwa wote walioteuliwa wamebobea katika masuala mbalimbali yanayohusu Elimu.
Akizungumza mara baada ya maelekezo ya Waziri Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Naomi Katunzi amemhakikishia Waziri Ndalichako kuwa bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia kanuni,  taratibu na miongozo iliyopo.
Dk. Katunzi amesema kuwa wamepokea kwa mikono miwili uteuzi huo na kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu Kati ya bodi na uongozi wa ADEM.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu  Dk. Siston Masanja amesema  bodi hiyo  itaishauri  ADEM katika masuala mbalimbali ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
Bodi hiyo ambayo imezinduliwa leo itatekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka Mitatu.
 
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
3/2/2018
Read 8899 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…