Jumatano, 17 Januari 2018 10:39

TAARIFA KWA UMMA: DIRAPLUS YATAKIWA KUACHA KUINGILIA MAJUKUMU YA TET

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatoa taarifa kwamba katika siku za hivi karibu kumejitokeza baadhi ya Taasisi zinazoingilia majukumu ya Taasisi kinyume cha Sheria.

Ikumbukwe kwamba TET ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambayo ilianzishwa kwa Sheria Na. 13 (1975) ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Sheria hii TET ndiyo Taasisi pekee nchini yenye mamlaka ya kubuni, kuandaa na kusambaza Mitaala na Mihtasari ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu.

Kwa masikitiko makubwa Wizara na Taasisi zimegundua kwamba Asasi inayojulikana kama DIRAPLUS imeamua kwa makusudi kuingilia majukumu ya msingi ya Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kubadili Mihtasari ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Sekondari na kuiweka kwenye mtandao wake. Mihtasari hii imewekwa kwenye mtandao huu bila idhini ya Taasisi ya Elimu Tanzania, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria za nchi.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania inaiagiza  DIRAPLUS kuondoa machapisho hayo ya mihtasari mara moja wakati Taasisi inaendelea na mchakato wa kisheria wa kushughulikia kadhia hii.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania inapenda kuwajulisha wadau wote wa Elimu na umma kwa ujumla kuwa mitaala na mihtasari ya shule kuanzia Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu inapatikana katika duka la vitabu ambalo liko katika ofisi za TET Mwenge, Dar es Salaam na katika mtandao wa TET wenye anuani http://www.tie.go.tz.

Imetolewa na:

Dkt. Aneth  Komba
Mkurugenzi Mkuu
TAASISI YA ELIMU TANZANIA 
Read 16193 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…