Jumamosi, 13 Januari 2018 10:54

TAARIFA KWA UMMA

YAH: KUWAREJESHA WANAFUNZI WALIOFUKUZWA, KUKARIRISHWA AU KUHAMISHWA SHULE KWA KUTOFIKIA WASTAN! WAUFAULU WA SHULE

Waraka wa Elimu Namba 7 wa Mwaka 2004 umepiga marufuku utaratibu wa  shule zisizo zaserikali kukaririsha Darasa, kufukuza au kuhamisha Mwanafunzi aliyefanya na kufaulu Mtihani wa Darasa la Nne,

Kidato cha Pili na Kidato cha Nne kwa kigezo cha wanafunzi hao kutofikia wastani waufaulu washule husika.

Waraka huo umeeleza wazi kuwa ni marufuku kufanya vitendo hivi vya kinyanyasaji kwa  wanafunzi, wazazi na walezi na kwamba shule yoyote itakayobainika kukiuka taratibu za Wizara itachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutoruhusiwa kusajili wanafunzi.

Pamoja na kutolewa kwa waraka  huo, hivi karibuni Wizara  imebaini kuwepo kwa baadhi ya shule zisizo za serikali  kukaririsha na kuhamisha wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu wa shule.

Aidha, baadhi ya wakuu wa shule wamefikia hatua ya kuwatuhumu wanafunzi kuwa na   makosa ya utovu wa nidhamu na kisha kuwaeleza wazazi au walezi wa mwanafunzi  husikakuwa adhabu ni kurudia darasa au kuwarejesha shuleni kwa masharti ya kuwatafutia shule/vituo vingine vya kufanyia Mitihani yao ya mwisho. Jambo hili ni kinyume na Taratibu na Sheria, Miongozo na Taratibu zilizowekwa na Wizara.

Kufuatia ukiukwaji huo wa  taratibu zilizowekwa na Wizaraya Elimu, Sayansina Teknolojia  kuanzialeo  tarehe  12 Januari, 2018 Wizara inaziagiza  shule  zote zilizokaririsha, kuhamisha au kufukuza  shule wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu washule kuwarejesha  shuleni  wanafunzi  hao    ifikapo  tarehe  20/1/2018  ili waendelee na  masorno   yao  katika    madarasa  ambayo  wanapaswa kuwepo kisheria na wahakikishe kuwa wanaandikishwa kufanyia Mitihani yao ya mwisho katika shule hizo na sio vituo tofauti.

Aidha,  Wazazi  na  Walezi  wa  wanafunzi  wote ambao    watoto wao walirudishwa  nyumbani wanapaswa kuwapeleka shuleni wanafunzi katika muda uliotajwa na Wizara ili wanafunzi waendelee na masomo yao.

Shule ambayo itakaidi agizo  hili,   Wizara itawachukuliwa hatua  za kisheria   ikiwemo kufungiwa usajili wa wanafunzi na kufutiwa usajiliwa shule.

Wizara   ya  Elimu,  Sayansi   na  Teknolojia  inapenda  kuwakumbusha wamiliki  nawaendeshaji wote wa Shule  kuzingatia Sheria, Miongozo na Taratibu zilizowekwa na Wizara.

Imetolewana:

KamishnawaElimu
Dkt.EdicomeC.Shirima
WizarayaElimu,SayansinaTeknolojia
12Januari,2018
Read 55795 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…