Jumanne, 07 Novemba 2017 04:39

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA ELIMU WAZIRI WA ELIMU ASHIRIKI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Elimu ya Ufundi ndiyo nguzo muhimu ya kufikia ajenda ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

 
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua kongamano la kimataifa la wadau wa Elimu ya Ufundi na mafunzo jijini Dar es salaam, na kusisitiza kuwa dira ya Maendeleo  ya 2025 imeipa Elimu kipaumbele cha juu kwa kuwa ndiyo Kitovu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
 
Makamu wa Rais amesema kuwa serikali kipitia baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi litaendelea kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo katika taasisi za Elimu ya Ufundi ili Taifa liwe na wataalamu wa kutosha na wenye weledi katika fani mbalimbali kwa Maendeleo ya Taifa.
 
Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo wa siku tatu ni pamoja na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Katibu Mkuu Dkt.Avemaria Semakafu, Wakuu wa Taasisi , na wadau mbalimbali.
 
Kauli mbiu katika mkutano huo ni Wekeza katika Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.
 
Imeandaliwa na;
 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
 
6/11/2017

 

Read 6404 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…